Na Mwandishi wetu Mihambwe
Wananchi wameaswa kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kuweka akiba, kuwekeza ama kufanya biashara ili kukuza uchumi wao.
Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati akizungumza kwenye mikutano ambayo imewashirikisha ugeni toka Benki Kuu ya Tanzania iliyofanyika Kata ya Mihambwe na Kitama.
“Mbele ya ugeni toka Benki Kuu ya Tanzania niliowaalika napenda niwasisitizie Wananchi juu ya nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kujiepusha na anasa badala yake mfanye ujenzi wa nyumba za kisasa, uwekezaji kwenye biashara na hata kuwekeza kwenye Elimu ya Watoto wetu.” Alisisitiza Gavana Shilatu
Ugeni huo kutoka Benki Kuu ya Tanzania ulikuja na ujumbe wa namna ya kutambua fedha halali; Elimu ya uhifadhi wa fedha kwa njia salama; na namna ya ubadilishaji wa fedha ambapo Wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa majibu.
Wakati huo huo Gavana Shilatu alitumia mikutano hiyo kuwasihi Wazazi wenye Watoto waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza kuwaruhusu na kuwapeleka shuleni Watoto wao kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Katika mikutano hiyo ilihudhuliwa na Watendaji wa Kata, halmashauri Serikali za Vijiji, viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya kisiasa.