Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwajelwa, akizungumza na na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana. |
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wakimsikiliza Dkt. Mwanjelwa.
……………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Singida
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwajelwa amesema Serikali baada ya kugundua kuwepo kwa uozo kwa watumishi mbalimbali wanaokaimishwa nafasi mbalimbali waliamua kuja na waraka unaoelekeza kikomo cha mtumishi kukaimu katika nafasi husika.
Mwanjelwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.
“Suala la kukaimu kwa muda mrefu ndiko kuna sababisha kuwepo na uozo mkubwa katika sehemu zetu za kazi kutokana na watendaji hao kutokuwajibika kwa ufanisi” alisema Mwanjelwa.
Naibu waziri huyo amewataka watumishi wote wa halmashauri hususani mkurugenzi na wakuu wa idara kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri wa kitaalamu unao tolewa na akasisitiza sauala la mafunzo katika kazi ili kuwaongezea ujuzi watumishi hao.
Katika ziara hiyo mbali na kukutana na kutatau kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za mkoa wa Singida pia anapitia kuangalia utekelezaji wa mpago wa kunusuru kaya Masikini TASAFKatika ziara hiyo mbali na kukutana na kutatau kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za mkoa wa Singida pia anapitia kuangalia utekelezaji wa mpago wa kunusuru kaya Masikini TASAF