RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamede Shein, akimsikiliza Msimamizi wa Mradi wa Jengo hilo Ndg. Peter Lazaro , wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Eng. Dkt. Idrisa Muslim Hija.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Konde wakiimba wimbo maalum wa kuwapongeza Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Wingwi Wilaya ya Micheweni Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais ) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na (kushoto kwa Rais ) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma.(Picha na IKULU)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamede Shein akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza Mtoto Fatma Hamad Juma,Mwanafunzi wa Skuli ya Msingi Konde aliyeshiriki katika kuimba wimbo Maalum na kutowa Salamu za Watoto wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Kijiji cha Wingwi wakifuatilia hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli hiyo.(Picha na IKULU)