Kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Desemba wa Ligi Kuu baada ya kuwashinda Juma Mgunda wa Coastal Union na Sven Vandenbroeck wa Simba
Kwa upande wa wachezaji Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Francis Kahata Nyambura amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2019/2020.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya amefanikiwa kushinda tuzo baada ya kuwashinda mchezaji mwenzake wa Simba, kungo pia Hassan Dilunga na beki Bakari Mwanyeto wa Coastal Union alioingia nao fainali.
.