RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa (ZAWA) Ndg.Mussa Ramadhani Haji akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Tangi la Maji Saateni Zanzibar, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi huo wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira uliofanyika leo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa (ZAWA) Ndg. Mussa Ramadhani Haji akitowa maelezo ya michoro iliopita mabomba ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (kulia kwa Rais) Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Zanzibar.Mhe.Salama Aboud Talib. Ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Saateni Wilaya ya Mjini Unguja, (kulia kwa Rais) Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati.Mhe. Salama Aboud Talib na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati.Ndg.Ali Halil na Mkurugenzi Mkuu wa (ZAWA)Ndg. Mussa Ramadhani Haji, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kulizindua Mradi wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika eneo la Saateni Jijini Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, (kulia kwa Rais) Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati.Mhe.Salama Aboud Talib na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyuma Maji na Nishati.Ndg. Ali Halil na Mkurugenzi Mkuu (ZAWA) Ndg. Mussa Ramadhan Haji.(Picha na Ikulu)