Baadhi ya wananchi na Waalikwa mbalimbali waliohudhuria Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni Rasmi katika Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Baloz Ali Abeid Karume akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
Mtoa mada Nd,Ali Shaaban akitoa mada kuhusu Maisha ya Sheikh Abeid Amani Karume katika Ufunguzi wa Kongamano la miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil kikwajuni Zanzibar.
………………
Na Mwashungi Tahir,Maelezo.
WAZIRI wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume amesema Serikali itaendelea kuwaelimisha vijana na kuhakikisha kwamba wanayaenzi na kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Miaka 56 ya Mapinduzi ya Matukufu ya Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya Mapinduzi hayo lililofanyika huko katika ukumbi wa Idrissa Abdul Wakil huko Kikwajuni.
Amesema vijana wanapaswa kuifahamu Historia ya nchi yao kwa lengo la kuyajua mambo yaliyotokea kabla ya Mapinduzi hadi kupatikana kwa uhuru na kujikomboa.
“Vijana kongamano hili litaweza kuona historia ya Mapinduzi tangu yalivyoanzia hadi kufikia kupata uhuru wa Nchi yetu”alisema Waziri Karume.
Alieleza kuwa wananchi ni vyema kuwakumbuka waasisi waliofanya Mapinduzi chini ya uongozi wake Jemedari Mkuu Marehemu Mzee Abeid Amani Karume aliyemkomboa Mzanzibar katika makucha ya kisultani na kumpatia uhuru.
Balozi Ali Karume alisema kuwa Lengo la kongamano hilo kuwaelimisha vijana na kuijua historia ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi pamoja na kumfahamu mwasisi Marehemu Mzee Karume jinsi alivyopigana na kuleta maendeleo nchini.
Aidha Balozi Karume alimpongeza Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wa awamu zilizopita kwa kuyaendeleza yale yote yaliyoasisiwa na marehemu Mzee Karume na kuleta maendeleo pamoja na kudumisha amani na utulivu nchini.
Balozi Karume aliwataka vijana hao kutosikiliza maneno ya wasiopenda maendeleo kwani Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika kihalali chini ya Jemedari Mkuu Marehemu Mzee Karume.
Mada mbili ziliwasilishwa ikiwemo Maisha ya Marehemu Mzee Karume na Mada ya Mapinduzi ya Zanzibar na Maendeleo ambapo Mshauri wa Rais katika mambo ya Historia na Mambo ya Kale Ali Mzee Ali, aliiwasilisha kwenye kongamano hilo linalo lengo la kuwaenzi wazee walojitolea muhanga katika kupigania uhuru kw a kumng’oa mkoloni na kupata maendeleo nchini.
Aidha aliwasisitiza vijana kuyaenzi Mapinduzi na kuyathamini kwani yameweza kuletea maendeleo kwa kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji safi na salama na miundombinu nchini.
“Mapinduzi ya Zanzibar yametuletea maendeleo makubwa hivyo ni vyema yazidi kuendelezwa kutunzwa na kuthaminiwa”, alisema Mshauri huyo.
“Vijana nawaombeni kufuata wasia aliyouacha Marehemu Mzee Karume kwamba tukuza kilicho chako na kusahau cha mwenzako, poteza maisha yako kwa kuokoa nchi yako”, alieleza Mshauri huyo
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Mjini Talib Ali Talib alishauri kutolewa kwa elimu ya Historia ya Zanzibar kwa vijana ili kuweza kutambua mambo yote yaliyotokea nchini.
Pia aliwataka wasanii kufikisha ujumbe wa mambo yaliyotokea kabla ya Mapinduzi hadi kupatikana uhuru wa Zanzibar kupitia michezo ya kuigiza ili jamii iweze kufahamu historia ilikotoka.