Home Michezo KISA SARE NA YANGA,MANARA ‘AWALIPUA’ VIKALI WACHEZAJI SIMBA

KISA SARE NA YANGA,MANARA ‘AWALIPUA’ VIKALI WACHEZAJI SIMBA

0

MSEMAJI wa Klabu ya Simba SC Haji Manara amewataka wachezaji wa timu hiyo kutambua thamani ya jezi yao na kujituma zaidi wawapo uwanjani kama wafanyavyo wapinzani wao wa jadi Yanga.
Manara ametoa ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Simba kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jana, akisema kuwa kuna baadhi ya wachezaji ‘waliboa’ jambo linalowapa Yanga jeuri ya kutamba mitaani.
“Wenzenu hawapati mnachokipata, wanapanda daladala hadi Mbeya, hawakai camp nzuri, hawalipwi kwa wakati, hawapati bonus mzipatazo lakini wanawazidi fighting spirit na commitment kwa mbali sana!!…. Kifupi baadhi yenu mmeboa mno!!” amesema Manara kupitia mtandao wa Instagram. 

Ameongeza kuwa kwa mchezao wa jana, Simba haikustahili matokeo ya sare, huku akiwabebesha lawama wachezaji kwamba wamewaangusha mashabiki, uongozi na bodi ya wakurugenzi chini ya mwenyekiti wake Mohamed Dewji.