Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti nyeupe) akitembelea na kukagua ujenzi wa zahanati ya Bushushu iliyopo katika kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga leo Januari 3,2020 wakati akiendelea na ziara yake Jimboni. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti nyeupe) akizungumza kwenye zahanati ya Bushushu na kuahidi kupeleka moramu kwenye zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (mwenye suti nyeupe) akipokea maelezo kuhusu ujenzi wa zahanati ya Bushushu ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na mbunge kuchangia mifuko ya saruji na sasa ujenzi umefikia hatua ya renta.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akikagua jengo la zahanati ya Bushushu.
Muonekano wa jengo la zahanati ya Bushushu.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rashid Mnunduma akizungumza wakati wa kikao cha Mbunge Stephen Masele na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Lubaga Anord Makombe akizungumza wakati wa kikao cha Mbunge Stephen Masele na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Lubaga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Kambarage wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata ya Kambarage.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Amri Migeyo wakati Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Kambarage wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Mjini wakati wa ziara yake leo Januari 3,2020.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mhe. Masele amefika katika zahanati ya Bushushu leo Ijumaa Januari 3,2020 ikiwa ni mwendelezo wa ziara katika Jimbo lake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wajumbe wa kamati za siasa CCM ngazi ya matawi na kata.
“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa zahanati ya Bushushu yenye vyumba 15 ambayo mimi mwenyewe niliuanzisha kwa kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji.Niwapongeze sana wananchi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wenu kushiriki ujenzi wa zahanati hii.
“Nimerudi tena kwa mara pili kuwaunga mkono wananchi ili tukamilishe ujenzi huu na wananchi waanze kupata huduma za afya. Nitaleta moramu kujaza jengo hili pamoja na kutafuta fedha lakini pia nitazungumza na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili amalizie ujenzi kwa kupaua jengo hili kwani sisi wananchi tumeshajenga boma. Kwa utaratibu uliopo wananchi wakijenga boma,serikali inatakiwa kumalizia ujenzi”,alieleza Masele.
Mbunge huyo alisema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara,maji na umeme huku akibainisha kuwa huwezi kuzungumzia maendeleo ya mji wowote bila kugusa miradi hiyo ambayo inahitaji mikakati mizuri kuitekeleza badala ya bla bla.
“Huwezi kutenganisha maendeleo ya Shinyanga Mjini na Mbunge wa Jimbo. Tunayo ‘Master Plan’ tuliyoitengeneza tangu mwaka 2011,Huu ni mkakati wa kuboresha mji wa Shinyanga uwe wa Kisasa. Utekelezaji wa awamu ya kwanza naweza kusema umeisha mwaka 2019 ambapo tumefanikiwa kujenga barabara za lami kilomita 13 za kupitia Benki ya dunia. Na katika awamu ya pili tunatarajia kujenga kilomita 18 za barabara za lami zingine mpya.
Hizi kilomita 13 za barabara tulizojenga hadi sasa tu zimeufanya mji wa Shinyanga upendeze kiasi hiki ambapo kuna barabara za lami na taa zake. Je tukiongeza barabara zingine kilomita 18 muonekano wa mji utakuwaje?,ndiyo maana nikisema tunataka Shinyanga iwe mji wa Kisasa kuna baadhi ya watu hawanielewi kwa sababu hawajui mipango iliyopo”,alifafanua Masele.
Masele alisema mpango uliopo ni kuhakikisha kata zote za Jimbo la Shinyanga Mjini zinaunganishwa kwa barabara za lami na kuwaomba wananchi kutumia fursa ya mji wa Shinyanga kufanya shughuli za kujiinua kiuchumi.
Mbali na kutembelea kata ya Lubaga, Mhe. Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini amekutana na Wajumbe wa kamati ya siasa Chama Cha Mapinduzi CCM wa ngazi ya matawi na kata ya Mjini na Kambarage.