Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akisalimiana na viongozi wakati akiwasili kwa ajili ya kufungua na kuzindua kituo cha mafuta cha Sheli ya Kampuni ya Admire Oil jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Admire Oil Bw.Said Mire Artan wakati wa kufungua na kuzindua kituo cha mafuta cha Kampuni ya Admire Oil jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akikunjuwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa Jiwe la Msingi Kituo cha Mafuta Kipya cha Kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akipiga makofi mara baada ya kuzindua Jiwe la Msingi la Kituo cha Mafuta Kipya cha Kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Msemaji wa Kampuni ya Admire Oil Bw.Mohammed Ibrahim,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akizugumza na wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Sehemu ya wananachi waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Hii ndo Sheli mpya ya kampuni ya admire Oil iliyofunguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,jijini Dodoma.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa kwenye foleni wakisubiri kujaziwa mafuta bure mara baada ya kufunguliwa kwa kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya admire Oil jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akimtazama meneja wa kituo hicho Bw.Faisal Abdalah akibonyeza ili mafuta yaanze kutoka katika kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akijaza mafuta kwenye bodaboda mara baada ya kuzindua kituo kipya cha mafuta cha kampuni ya Admire Oil kilichofunguliwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya admire Oli mara baada ya kuzindua kituo kipya cha mafuta.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG
………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wote wa maendeleo ambao wanawekeza nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki kwao.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde,alipokuwa akizundua pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha mafuta cha Amire Oil inayofanya biashara ya mafuta mikoa mbalimbali nchini.
Mhe Mavunde amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli inathamini wawekezaji kutokana na mchango wao katika kutoa ajira na kukuza pato la Taifa kupitia kodi wanazolipa.
” Niupongeze uongozi wa Kampuni hii kwa kukuona umuhimu na ulazima wa kuja kuwekeza katika Jiji la Dodoma kwani kufanya hivyo kutaongeza fursa kubwa za ajira kwa vijana ikizingatiwa tayari mmeshaajiri ajira 20 mpaka sasa kwa wananchi wa Dodoma.
Sisi kama Serikali tunaendelea kutoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza katika Jiji hili ambalo ndio Makao Makuu ya Serikali lakini pia kuna maeneo mengi ya Uwekezaji na rafiki kwa ajili ya kujenga viwanda, hoteli na hata majengo ya kibiashara, ” Amesema Mhe Mavunde.
Awali Msemaji wa makampuni ya Admire Oil Bw.Mohamed Ibrahim ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji jambo ambalo linaongeza ari kwao ya kuzidi kufanya Uwekezaji katika maeneo mengi zaidi nchini.
” Kwa kweli serikali ya Rais Magufuli imetoa mazingira rafiki sana kwa wafanyabiashara hasa wazalendo. Sisi tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali yetu ili kufikia ndoto ya Rais wetu ya Tanzania ya viwanda.
Tunafahamu lengo la kila mfanyabiashara ni kuwekeza na kupata faida lakini kampuni yetu ya Admire moja kati ya malengo yake makubwa ni kugawa ajira kwa akina Mama na vijana wengi nchini, ” Amesema Ibrahim.
Aidha amesema kuwa wameajiri vijana wengi sana takribani watu mia moja na hamsini nchini na kati ya hao wengi wao ni wanawake ili tu kuwainua pamoja na kuwawezesha kiuchumi.
Kampuni ya admire Oil ina matawi mengi katika mikoa mbalimbali nchi kituo kikubwa kikiwa ni mkoa wa Pwani pamoja na mikoa ya Mwanza,Arusha,Mbeya,Dar es Salaam na Dodoma tunapatikana katika huduma ya mafuta.