******************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Jeshi la polisi mkoani Kagera limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kuelekea mwishoni mwa mwaka na kuonya baadhi ya watu ambao watataka kuvunja amani kwani watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake RPC Malimi amesema kuwa hali ya usalama katika mkoa huo umeimalika hivyo amewaonya baadhi ya watu watakaojaribu kuhatarisha amani kwa raia kuchukuliwa hatua.
Aidha RPC Malimi amesema kuwa mwaka 2018 makosa dhidi ya binadamu yalikuwa 427 ukilinganisha na makosa 432 yaliyotokea mwaka 2019.
“Kulikuwepo na ongezeko la makosa ya kibinadamu kwa mwaka 2018 kama mauaji,kubaka,kulawitiwa,wizi Wa watoto na utupaji Wa watoto ambapo ametaja chanzo cha makosa hayo nimigogoro ya mashamba au Mali za urithi, wivu wa mapenzi, kulipa kisasi,ugomvi unaotokana na ulevi pai na kiasi kidogo cha imani za kushirikina”. Amesema RPC Malimi.
Hata hivyo amewataadhalisha wananchi kuwa makini hasa kipindi hiki cha mwaka unapoelekea kuisha amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa watakapoenda katika fukwe za ziwa Victoria wasiwaache watoto kuogelea peke yao.
” Mzazi ni jukumu kumlinda mtoto wake kwahiyo tutaimalisha ulinzi tutakuwa na jeshi la uokoaji majini lakini pia tutaimalisha usalama hats katika mitaa yetu na Barbara zote zinazotoka mjini na kuingia na hata vijijini lakini zile kumbi za starehe kwa kwa watoto azitakuwepo maana tumekagua kumbi zote lakini azina vigezo”
Sambamba na hayo ameyataja mafanikio mbali na kuwepo kwa baadhi ya matukio yaliyotokea 2019 lakini amesema kuwa jeshi la polisi limepambana na uhalifu vya kutosha ambapo jeshi hilo limafanikiwa kukamata silaha za kivita toka mikononi mwawahalifu waliokuwa wamepanga kuzitumia katika utekaji na nyingine wakizimiliki isivyo halali ambazo ni Ak-47, risasi 17, short gun 02, na magobole 02.