Home Mchanganyiko PWANI YAPUNGUZA AJALI KWA ASILIMIA 7.3 PIA YAENDELEZA MSAKO WA NYAKUANYAKUA

PWANI YAPUNGUZA AJALI KWA ASILIMIA 7.3 PIA YAENDELEZA MSAKO WA NYAKUANYAKUA

0

******************************

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani,umepunguza ajali za barabara kwa asilimia 7.3  ,ambapo mafanikio hayo yametokana na kufanyika operesheni mbalimbali na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara.
Aidha mkoa huo,unaendelea na operesheni nyakuanyakua madereva korofi na wazembe ambayo imeanza mwanzoni mwa mwezi desemba na itakamilika mwezi januari 2020.
Akizungumzia malengo na mikakati ya kudhibiti ajali mkoani hapo, mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani Pwani, Mosy Dozero alisema ,kipindi cha nyuma kutokea ajali moja ama ajali inayosababisha majeruhi na kifo  ilikuwa ni jambo ambalo halipingiki lakini kwasasa inaweza kupita wiki nzima kusitokee ajali.
Mosy alieleza kuwa, wamejipanga kukomesha ajali zembe na kuendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara kwani PWANI BILA AJALI YAWEZEKANA.
Nae kamanda wa polisi mkoani humo,(ACP) Wankyo Nyigesa alifafanua, takwimu zinaonyesha kuwa tumefanya vizuri mwaka 2019 ,ukilinganisha na mwaka 2018 ,ambapo makosa ya ajali zilisababisha vifo mwaka 2018 yaliripotiwa 41 , mwaka huu 2019 ajali zilizosababisha vifo zilikuwa 32″:aliweka bayana Wankyo.
Wankyo alibainisha, makosa ya ajali zilizosababisha majeruhi kwa mwaka jana 2018 ziliripotiwa 100 mwaka huu ajali ziliripotiwa 64.:
Alitoa wito na kuwataka watumiaji wa vyombo vya moto,magari,pikipiki,bajaji,toyo na watembea kwa miguu kuendelea kutii sheria za usalama barabarani kwakuwa atakaekiuka sheria hizo atachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani.
Wakati huo huo kamanda huyo ,amepiga marufuku kwa mtu yeyote au taasisi ya serikali kufyatua fataki siku ya mkesha wa mwaka mpya bila kibali cha Jeshi la polisi.
Wankyo anasema, ni marufuku kuchoma tairi katika barabara za umma ama mitaani kwa kufanya hivyo utakuwa umekaribisha Jeshi la polisi kukukamata na kukupeleka mahakamani.