Na Silvia Mchuruza. Bukoba.
Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi CCM taifa Dr.Bashiru Ally amewataadhalisha wanachama na viongozi wote kuwa serikali ya chama cha mapinduzi haitatoa fedha yoyote au kutoa sare ya chama bure kwa wanachama ikiwa uchaguzi gharama zake ni ndogo.
Akizungumza na viongozi wa chama katika ukumbi wa chama cha mapinduzi mkoa wa kagera Dr.Bashiru amesema kuwa uchaguzi ujao akutakuwepo na kitu chochote cha bure si kwa mwanachama au mgombea kutokana na kutoitaji misaada kwa watu ambao wamekuwa wakikwepa kodi.
Hata hivyo ameongeza kuwa chama akitaitaji msaada wowote kutoka kwa watu wenye uwezo mkubwa kutokana na baadhi ya watu hao kutolipa kodi ambayo inalinufaisha taifa na jamii kwa ujumla kama kuimalisha miundombinu.
“Nataka kuwasisitiza kwamba msitumie misaada ya masharti kuendesha uchaguzi kutokana na uchaguzi unaitaji pesa lakini pesa iliyo halali na kutafuta dola siyo kitu cha mchezo na uchaguzi siyo msimu Wa mapato na kipi cha uchaguzi huwa nikama vita ya kuimarisha dola ya chama chako na mkumbuke mjiandae kutafuta pesa zenu wenyewe kuendesha uchaguzi na mjiandae oia kufanya uchaguzi usiyo Wa gharama”
Aidha amewataka wagombea kufanya kazi yao kwa kujituma lakini pia amewataka kuwa na nidhamu nakutunza siri za chama na maamuzi ya vikao na pia amesema kuwa ni mwiko kwa viongozi kuvujisha siri za chama katika mitandao ya kijamii.
“Nawasisitiza kuwa makini na kutovujisha siri za vikao maana unakuta mtu anahukumiwa na kusemwa mitandaoni ikiwa yeye hawezi kukiteta tunatakiwa kuwa na nidhamu katika chama” alisema” Dr.Bashiru.
Sambamba na hayo amewashukuru viongozi na wanachama kwa ujumla kutokana na kuwa na ushirikiano lakini pia ameongezea na kusema kuwa serikali hii ya awamu ya tano imefanya kazi mkubwa sana has a katika elimu na miundombinu.