Na.Ashura Mohamed -Arusha
Wataalamu wa Mionzi nchini wametakiwa kuwa na weledi na kuongeza umakini katika matumizi ya mionzi salama ili kuhakikisha kuwa watanzania wanabaki salama.
Kufuatia Hali hiyo ambayo inaelezwa kuwa sheria na taratibu zikifutwa hospitali nyingi hapa nchini zitaepuka adha ya kufungiwa ikiwa zitakuwa na mashine zenye ubora pamoja na watoaji wa huduma za mionzi waliobobea.
Kutokana na sheria kukiukwa jumla ya hospitali 94 ambazo zinatoa huduma za Mionzi nchini zimefungiwa kutokana na kutokidhi ubora wa utoaji huduma hiyo hapa nchini.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo ya siku tano ya Uthibiti Usalama wa Mionzi katika idara ya radiolojia nchini yaliyofanyika katika Kituo cha nguvu ya Atomik jijini Arusha Mkurugenzi wa kituo hicho Profesa Lazaro Busagala alisema jumla ya hospitali zilizofanyiwa Ukaguzi ni 664 ambapo hospitali 105 zilifungiwa kutokana na kutokukidhi vigezo vilivyopo.
Profesa alisema kuwa mara baada ya ukaguzi Hospitali kumi tu zilifunguliwa kutokana na kukidhi vigezo na kufunguliwa ambapo mpaka sasa 95 bado zimefunga kwa mujibu wa kaguzi za mwaka 2019/2020.
Aidha aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanatumia vyema taaluma zao katika kuhakikisha kuwa watanzania haawaathiriki na Mionzi na pindi ambapo wanaona kuna changamoto katika maeneo yao ya kazi basi waweze kuhakikisha kuwa wanashauri kwa kutumia maandishi na sio maneno.
“Tutachukua hatua kali kwa wakuu wa hospitali ambazo hazitafuata taratibu tutafungia moja baada ya nyingine mpaka taratibu zitakapofuatwa ili watanzania waweze kuwa salama”alisema profesa Busagala
Kwa Upande wake Mkurugenzi Uthibiti na Usimamizi na Matumizi Salama ya Mionzi Dkt.Justine Ngaile alisema kuwa baadhi ya mapungufu ambayo yanapelekea hospitali hizo kufungwa ni pamoja na kukosa mtaalamu ambaye ana ubora wa kutoa huduma hizo lakini pia Ubora wa mashine ambazo zinatumika kwenye huduma ya mionzi kutokuwa na ubora ikiwa ni pamoja na Jengo linalohidhi mionzi kutokuwa na ubora wa kutosha.
Hata hivyo dkt.Ngaile alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa mionzi hatarishi haiwezi kuwafikia wataanzania na kuwaletea Athari bali wawe katika mikoni salama na kuhakikisha kuwa wataalamu wanaongezewa ujuzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa teknolojia na Ufundi Filmi Banzi alisema kuwa Tanzania ipo salama kwa kuwa tume ya nguvu za atomic ina ofisi zipatazo 26 mipakani kwa nchi nzima ili kuzui vyanzo holela vya Mionzi ambavyo havihitajikikwa kutumia vifaa maalum ambavyo ni gunduzi kwa mionzi isiyo salama.
Faustine Mulyutu ambaye ni katibu wa wataalamu Mionzi Mikoa ya Tanzania Bara aliiomba serikali kuhakikisha kuwa sekta ya wataalamu wa picha za mionzi inapewa kipaumbele kama nyinginezo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi uliotukuka.
Jumla ya wataalamu wapatao 104 wamehudhuria mafunzo hayo wakiwa ni pamoja na mariadiojia,madaktari,na wauguzi ambao wanahusikaa na namna moja ama nyingine na mionzi ya mahospitalini.