Na.Ashura Mohamed -Arusha.
Wachimbaji,madalali na wafanyabiashara wa Madini Mkoa wa Arusha wamemwaomba Waziri Wa Madini Dotto Biteko leseni za Kanda zitumike nzima ili kuuza Madini ya aina mbalimbali Kwa Mataifa mengine.
Wameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa Madini uliohudhuriwa na wafanyabiashara,madalali na wachimbaji pamoja na vyama vya wachimbaji mmoja wa wachimbaji hao Samweli Rugamalira Amesema nitakribani miaka 8 tangu aanze kazi hiyo ya uchimbaji Madini aina ya Tanzanite ,ameiomba wizara kuangalia namna ya kuziboresha na ziweze kutumia Nchi nzima.
Alieleza changamoto ya ajira ndani ya machimbo ya mererani jambo ambalo limeibua mjadala kwa wafanyabiashara wanaochimba madini kuwa ni lazima walipie shilingi milioni 400 hadi 500 jambo ambalo limeonekana kuleta utata, nakumowmba waziri biteko kuingilia kati .
kwa Upande wa madalali akiwemo Tupilike Samson Mwangosi aliiomba Wizara kuwatambua na kuwapatia ofisi ili kuweza kutekeleza kazi zao mana wamekuwa wakifanyabiashara kwa njia ya mali kauli jambo ambalo linafifisha utendaji wao nakuiomba Tume na wizara kusaidia.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa Madini Tanzania(Tamida) Sammy Mollely alisema wapo tayari kuongeza thamani ya Madini nchini lakini bado kunachangamoto ya ya vikwazo vya vibali kwa wataalamu wa usanifu,ungarishaji,na uwekaji wa Urembo(nakshi) kuchukuwa muda Mrefu pindi wanapoomba uku matarajio yao nikupata wataalamu kutoka nchi ya Srilanka ili kuongeza Ujuzi.
Sammy alisema kuwa uwepo wa Tasac imekuwa kikwazo kikubwa na kueleza na kero kwao hali inayochangia kudidimiza uchumi wa nchi,kwani uchukuwa Miezi 2 kupata kibali kusafirisha madini nakueleza ikiwezekana Tasac Ingeondolewa kwani haina msaada kwao.
Naye Mbunge wa Simanjiro James Olemilya alisema wilaya hiyo ndiyo kitovu cha uchimbaji wa madini lakini bei ya Madini ya Tanzanite imeonekana kuyumba nakuiomba wizara kufanyika uchunguzi wa kina nakubahini kilichojificha ili kuwabahini watu wanaochezea bei ya Tanzanite na kutokuipatia Nchi Hasara ..
Waziri wa Madini Mh Dotto Biteko amesema wafanyabiashara wa sekta ya Madini wanayo changamoto yakuifata njia isiyosahihi nakujikuta wanatoka nje ya Mstarikibiashara ,jambo ambalo amesisitiza kufuata hatua zaki sheria kwani sekta hiyo haiwezi kusimamiwa na Waziri mwenyewe uku serikali ikitaka uwazi wakibiashara na kuhitaji fedha ili kuweza kutekeleza Huduma zakijamii .
Biteko ameongeza kuwa Mheshimwa Rais Wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Maguguli Anandoto kubwa yakuifikisha Nchi katika Uchumi wakati na anachukizwa na mfanyabiashara anayetorosha Madini na kukwepa kodi ,na kusissitiza serikali inataka kuvutia wageni kuja kununua Madini kwa haki Nchini.
Naibu Waziri wa Nchi,ofisi ya Waziri mkuu, Sera,bunge kazi, Vijana,na wenye Ulemavu Mh Antony mavunde Amesema nchi inawahitaji wataalamu wa Madini kwa Asilimia kubwa kutoka Nchi ya Kenya na Srilanka ,nakuanzia mwakani Wizara yake itaanza kuliwekea mikakati katika uratibu wa wa vibali vya kazi kwa Wageni ,nakueleza kuwa katika kutatua changamoto ya vibali Vya kazi wizara imekuja na Mfumo mtandao wakupata Kibali cha kazi ili kuondoa urasimu nakupiga marufuku kwa watu wa kati kama waleta maombi, nakuwataka wafanyabiashara kupeleka wenyewe maombi yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe amepongeza utaratibu huo wa Mkoa kukutana na wadau wa Madini kusikiliza kujadili na kutatua changamoto zao na kuongeza wigo mpana wakibiashara ndani na nje ya Nchi nakusisitiza chama kitaendelea kuunga mkono serikali na kutekeleza ilani ya ccm ikiwemo wachimbaji kunufaika na sekta hiyo katika kuongeza mapato kwani ndiyo dhamira kuu ya serikali kua na soko kubwa la Madini kimataifa duniani.