Home Siasa NEC YATANGAZA TAREHE YA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

NEC YATANGAZA TAREHE YA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

0

Na Mwandishi Wetu,Songea

TUME ya Taifa ya Uchaguzi,imetangaza kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la  kudumu la wapiga kura  katika mikoa ya Ruvuma,Njombena Zanzibar litaanza rasmi tarehe 30 Desemba 2019 hadi tarehe 5 Januari 2020.

Hayo yamesemwa jana na mwakilishi wa Mkurugenzi wa tume hiyo Bakari Msenga wakati wa Mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa mjini Songea.

Katika mkutano huo uliwashirikisha viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini,wawakilishi wa Asasi za kirai,makundi maalum ya walemavu,vijana,wanawake,wazee na waandishi wa Habari ambapo alisisitiza kuwa, makundi hayo yana nafasi kubwa katika kuleta maabadiliko chanya na mwamko wa kimaendeleo katika jamii.

Aidha alisema, katika zoezi la uandikishaji  wa wapiga kura Tume ya Uchaguzi imetoa vibali kwa watazamaji mbalimbali wanaofuatilia zopezi zima la  uandikishaji wa  wapiga kura.

Awali Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Meristala Longway alisema, Tume imekamilisha maandalizi kwa ajili ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika kundi la mkoa wa Ruvuma,Njombe na Zanzibar.

Alisema, nchi yetu ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020,kwa hiyo zoezi  la Uboreshaji wa wa Daftari la kudumu la wapiga kura ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Kwa mujibu wake,zoezi la uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura nchi nzima  lilianza kufanyika tangu mwaka jana,ambapo mikoa 18 imekamilisha zoezi hilo na lengo ni kuona kama vituo hivyo bado vipo na kama vina sifa na hadhi ya kuwa vituo vya kujiandikisha wapiga kura kwa mujibu wa sharia kanuni za uchaguzi.

Alisema, kutokana na uhakiki huo,vituo vya kujiandikisha wapiga kura kwa nchi nzima viliongezeka kutoka 36,549 hadi 37,407,lakini katika mkoa wa Ruvuma vituo hivyo vimeongezeka kutoka 1,083 mwaka 2015 hadi kufikia 1,129 mwaka 2019.

Hata hivyo baadhi ya wadau wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wameitaka tume hiyo kubadili lugha yake kutoka Kiingereza na kuwa lugha ya Kiswahili hili Watanzania wengi waweze kufikiwa na kuelewa sharia za Tume hiyo.

Martin Mlata alisema, Tume itaendelea kutumia lugha ya Kiingereza katika sharia zake kuna uwezekano mkubwa wa wadau kutopata na kuelewa sharia hasa ikizingatia kuwa Watanzania wengi wameishia daras la sana na hawaelewi Kiingereza.