Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa juu ya mbinu za ulizni wa watoto hasa kwenye ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Lengo likiwa ni kuangalia namna gani asasi za kiraia zinaweza kufanya kazi kwa pamoja na viongozi wa dini kutokomeza ndoa za utotoni na mimba za utotoni, Semina hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam.
Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki akifurahia jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa juu ya mbinu za ulizni wa watoto hasa kwenye ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Mwezeshaji wa semina hiyo Mwanasheria Jones John akiwasilisha mada na taarifa ya tafiti mbalimbali barani Afrika zinazoonyesha matukio ya ndoa za utotoni na mimba za utotoni ambapo nchi kama Tunisia imepiga hatua katika kuzuia ndoa za utotoni na mimba za utotoni ukilinganisha na mataifa mengine kama Niger ambayo ina kiwango kikubwa cha matukio hayo.
Mwezeshaji wa semina hiyo Mwanasheria Jones John akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada na taarifa ya tafiti mbalimbali barani Afrika zinazoonyesha matukio ya ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Baadhi ya viongozi wa dini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Viongozi wa dini wanawake pia walihusishwa katika semina hiyo Mwanamke anachukuliwa kama nguzo muhimu katika kujenga familia iliyobora na inaweza kuleta manufaa katika taifa lolote lile.
Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki katikati akijadiliana jambo na mmoja wa wanasheria wa TAWLA Bi Subira wakati semina hiyo ikiendelea.