Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati) akiongozwa na Afisa Utumishi, Bakari Maulid Bakari
(kulia) kutembelea Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba. Kushoto ni Mhasibu kutoka Ofisi hiyo Mohamed Said Mwinyi.
Afisa Utumishi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar Bakari Maulid Bakari (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu shughuli za ofisi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene. Wengine kushoto ni Mhasibu Mohamed said Mwinyi na kulia ni Mratibu Othman Haji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiagana na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Zanzibar kabla ya kuelekea Pemba kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akipokewa na Mratibu wa shughuli za Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Othman Kassim Haji mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba.