Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro De Oliveira kwenye ofisi za Wizara ziliopo mji wa serikali mtumba jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao Waziri Ummy ameiomba nchi hiyo kutumia fursa ya kuingia kwenye manunuzi ya pamoja ya dawa na vifaa tiba kwa nchi za SADC kupitia bohari ya dawa nchini (MSD).
Aidha, amemuelezea Balozi huyo juu ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya viuadudu (Biolarvicides) kilichopo Kibaha ambacho kinazalisha lita zipatazo milioni sita kwa mwaka . Dawa ya viuadudu inayozalishwa na Kiwanja hicho Ina uwezo wa kuua mazalia ya wadudu dhurifu pamoja Na mbu waenezao
Malaria, Homa ya Dengue, ugonjwa wa chikungunya,homa ya bonde la ufa,Zika na wengineo pamoja na kuongeza kasi ya kudhibiti na kuondoa malaria katika nchi yao.
Vilevile, majadiliano hayo yalihusisha maeneo ambayo Tanzania Na Angola zitashirikiana katika kuwajengea uwezo wataalam wa Afya ili watoe huduma bora kwa wananchi