Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga akiongea na wanachama wa Chama wa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mtwara na Lindi kuwaelimisha kuhusu mpango wa Mfuko huu kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia makundi maalum na Vifurushi vya Bima ya Afya, leo 18.12.2019 Mkoani Mtwara
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Hipoliti Lello akiwasilisha mada kwa wanahabari wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuhusu mpango wa Mfuko huu kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia makundi maalum na Vifurushi vya Bima ya Afya, leo 18.12.2019 Mkoani Mtwara
Wanahabari wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga wakati wa mkutano na wataalam wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhusu mpango wa Mfuko huu kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia makundi maalum
Wanahabari wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia uwasilishaji wa mada wakati wa mkutano na wataalam wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhusu mpango wa Mfuko huu kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia makundi maalum na Vifurushi vya Bima ya Afya, leo 18.12.2019 Mkoani Mtwara
……………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, MTWARA
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amesema kuwa utaratibu wa vifurushi vya bima ya afya hauondoi taratibu mbalimbali zilizowekwa na serikali za kugharamikia matibabu kwa watu wasiojiweza ikiwemo wazee.
Bw. Konga amesema hayo leo Mkoani Mtwara wakati wa Mkutano na wanachama wa Chama wa Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Lindi na Mtwara walimpotaka atolee ufafanuzi wa kwanini gharama za matibabu kwa wazee katika vifurushi vipya vya bima ya afya ni tofauti na makundi mengine.
“Utaratibu unasema hivyo, hata Sera ya Afya ya Mwaka 2007 ukurasa ya 29 inasema serikali inatambua uwepo wa watu wasio na uwezo kutoka makundi ya, watoto, wazee na kina mama wajawazito, utaratibu huu unalenga wazee wenye uwezo na hauondoi taratibu za serikali za kugharamia makundi hayo ndio maana utaratibu wa msamaha kwa makundi hayo bado upo na unaendelea kama kawaida.
Aidha Bw. Konga amesema kuwa viwango vyake ni tofauti kutokana na hali halisi kuwa kadiri umri unavyokwenda mahudhurio ya hospitalini yanaongezeka na uhalisi wa gharama za matibabu zinakuwa kubwa zaidi.
“Utaratibu huu hauangalii uwezo wa kulipia fedha. bali unaangalia uhalisi wa gharama za matitabu, matatizo ya figo, matatizo na moyo mara nyingi yanakuwa kwa watu wenye umri kuanzia miaka hamsini na kuendelea, leo hii ugonjwa mfano wa tezi dume, gharama zake ni kubwa sana”-Bw. Konga
Akiongea wakati wa kuwasilisha mada kwa wanahabari hao Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja Bw. Hipoliti Lello amesema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha kila mtanzania anajiunga na bima ya afya na ndio maana mfuko umekuja na utaratibu wa vifurushi vyenye gharama kuanzia Laki moja na Tisini na Mbili.
“Awali tulikuwa na utatibu wa Milioni Moja na Nusu kujiunga kwa mtu mmoja lakini ilikuwa ni changamoto kubwa kwa mtu mmoja mmoja na ndio maana tumeishusha hadi kufikia laki moja na tisini na mbili, hii yote ni dhamira ya dhati ya kuhakikisha tunamrahisishia Mtanzania kujiunga na bima ya afya”-Bw. Lello.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Christopher Mapunda amesema kuwa tangu kuanza kwa vifurushi hivi muitikio wa watanzania umekuwa ni mkubwa hasa baada ya kupunguzwa kwa bei na hii imeonyesha kuwa huduma za bima za afya zilikuwa na uhitaji mkubwa