Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akikagua Gwaride
lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza
lililofanyika Desemba 17, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji
Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni alipowasili katika Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Tanzania tayari kwa hafla ya ufungaji Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi
la Magereza leo Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akiwa katika jukwaa kuu
tayari kwa kupokea salaam ya heshima kutoka Gwaride lililoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa
Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza lililofanyika Desemba 17, 2019 katika
Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni (kushoto) akimvisha cheo cha
Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa
Jeshi la Magereza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo.
Baadhi ya Maafisa toka Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wageni waalikwa meza kuu wakifuatilia Gwaride la wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa Wahitimu.
Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joel Matani akiwa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama
wakifuatilia Sherehe za ufungaji mafunzo hayo ya Uongozi ngazi ya juu, leo Desemba 17, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).