Home Michezo RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AIPONGEZA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR KATIKA...

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AIPONGEZA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR KATIKA HAFLA YA CHAKULA MAALUM ALICHOWAANDALI IKULU LEO

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco, wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu hiyo katika chakula maalum alichowaandalia Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco akizungumza na kuwatambulisha Wachezaji wa Zanzibar Heroes walioshiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji yaliofanyika Nchini Uganda, wakati wa hafla ya chakula maalum walichoandaliwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohammed Shein akiwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes baada ya hafla ya chakula cha maalum alichowaandali leo Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) .

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Washauri wa Rais waliosimama nyumba, waliokaa (kutoka kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar.Mhe Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi.Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee,Kadhi Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Saleh Omar Kabi na Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi,MheMgeni Hassan Juma, Waziri wa Michezo Vijana Sanaa na Utamaduni Mhe.Ali Karume na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe. Hassan Khatib Hassan.(Picha na Ikulu)

WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo picha) katika chakula maalum alichowaandalia katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa kuwapongeza kwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji yaliofanyika Nchini Uganda.(Picha na Ikulu)