Mchezaji Ally Mcharo wa Klabu ya TPC akipokea kikombe cha ushindi kutoka kwa Mwenyekiti wa Klabuya lugalo Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mstaafu aliyekuwa mgeni rasmi baada ya kupiga mikwaju Gross 160 kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro
Mshindi wa pili wa mashindano ya wazi ya Gofu Morogoro open Zacharia Edward wa Klabu ya Lugalo akipokea kikombe cha ushindi wa pili kutoka kwa Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo aliyekuwa Mgeni rasmi katika shereza za utoaji zawadi na Kufunga Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro mwisho wa wiki.
Mchezaji Vicky Elias wa Klabu ya Lugalo akipokea kikombe cha ushindi wa kwanza kwa waknawake kutoka kwa Mwakilishi kutoka Orynx Cira Muhele baada ya kupiga mikwaju 155 kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro.
Mashindano ya wazi ya gofu Morogoro yamemalizika huku mchezaji Ally Mcharo wa Klabu ya TPC akiibuka na ushindi baada ya kupiga mikwaju Gross 160 kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro.
Mshindi wa pili ni Zacharia Edward wa lugalo ambaye alipiga Mikwaju 161 huku upande wa Mikwaju ya Jumla Net kwa Divisheni A Mshindi ni Michael Mtweve wa Mufindi aliyepiga mikwaju ya Jumla 155 akifuatiwa na Maurus Kajuna wa Lugalo.
Katika Divisheni B Mshindi wa Kwanza kwaa Mikwaju ya jumla ni Amadi Rajabu wa Dar es salaam Gymkhana akifuatiwa na Teddy Kalinga wa Lugalo huku Divisheni C Mshindi ni Rory Mickllem wa Morogoro Gymkhana akifuatiwa na Musa Joseph wa Mufindi.
Kwa upande wa Wanawake Mshindi ni Vicky Elias wa Lugalo akifuatiwa na Joyce Warega naye wa Lugalo huku kwa Upande wa watoto ambao ni wa Morogoro pekee walichuaana na Mshindi ni Robert Colnelius huku mshindi wa pili ni Rajabu Omary na aliyepiga mpira mrefu ni Ally Mcharo na Hadija Selemani na waliopiga mpira jirani ni Zacharia Edward na Edna Chiwinga.
Akifunga Mashindano hayo Mgeni rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu alitaka klabu kuendeleza ushirikiano wa karibu na kuelekea kwenye maridhiano ya wachezaji wanachama wa klabu moja kuruhusiwa kucheza katika Klabu Nyingine bila Gharama.
“ Ili kuendeleza Mchezo hakuna Sababu mwanachama kulipishwa kila Sehemu ikiwa ni familia Moja hivyo Lugalo itaanza na Morogoro Gymmkhaana na Bilaa Shaka vilabu vingine navyo vinaweza kuunga Mkoano” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Pia alisema katika Mpango wa kukuza Vipaji Lugalo inatarajia kufikisha Idadi ya watoto 70 hivyo vilabu vingine navyo vianze kwa wananchama kwenda klabu zao na watoto wao kabla ya kushawishi watoto wengine iii kuibua vipaji vipya.
Aidha alisema Lugalo ipo tayari kutoa usaidizi wa kufundisha walimu wa Michezo katika mashule ya serikali iwapo Serikali itaamua na kuwaelekeza kwani ni klabu ya Jeshi kutoka Serikalini ni maelekezo naa Klabu iko Tayari muda Wote.
Kwa upande wake mwakilishi wa Chama cha gofu Tanzania Enock Magile amepongeza vilabu Vyote vilivyoandaaa Mashindano Mwaka 2019 na kuongeza kuwa Kalenda Kwa Mwaka 2020 imekamilika ni matumaini ya TGU mashindano yatafanyika kwa viwango zaidi ya Mwka uliopita.
Naye makamu mwenyekiti wa Morogoro Louis Roussos alishukuru Lugalo na wachezaji wengine kwa ushirikiano ikiwemo wa kiufndi katika kufanikisha mashindano hayo ambayo yanafunga mwaka kwa mujibu wa kalenda ya TGU.