Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia kwa waliosimama kwa nyuma), Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) wakishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano Jijini Dodoma baina ya Kampuni ya PT Wijaya Karya (WIKA)ya Indonesia na Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA-Afrika) mapema leo tarehe 17 Desemba, 2019 Jijini Dar es Salaam. Wanaosaini makubaliano hayo ni Mtendaji Mkuu wa WIKA Bw. Destiawan Simeon (kushoto) na Katibu Msaidizi wa CPA Afrika Bw. Said Yakubu.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA Afrika) Bw. Said Yakubu (kulia) akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PT Wijaya Karya (WIKA)ya Indonesia Bw. Destiawan Simeon (kushoto) mara baada ya kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya Nyota tano Jijini Dodoma. Utiaji saini wa makubaliano hayo yalishuhudiwa na Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia), Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) waliosimama kwa nyuma.
Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kulia) akizungumza na Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan walipokutana kwa ajili ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano mbalimbali ya uwekezaji Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji wa Indonesia, Mhe. Luhut Binsar Panjaitan (katikati) akizungumza na Waziri wa Uwekezaji wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki wakati walipokutana kwa ajili kushuhudia utiaji saini makubaliano mbalimbali ya uwekezaji Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA BUNGE