Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia,William Ole Nasha, akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti kwa washindi wa kitaifa shindano la uandishi wa insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kupitia wanafunzi wao jijini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Elimu hapa nchini Mwalimu Augusta Lupokela,akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti kwa washindi wa kitaifa shindano la uandishi wa insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kupitia wanafunzi wao jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia,William Ole Nasha,akitoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda shindano la kitaifa la Uandishi wa Insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kupitia wanafunzi wao jijini Dodoma.
Mratibu wa Uandishi wa Insha Sylvia Chinguwile,akitoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda shindano la kitaifa la Uandishi wa Insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kupitia wanafunzi wao jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia,William Ole Nasha,akiwa katika picha ya pamoja na wanafuzni walioshinda shindano la kitaifa la Uandishi wa Insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kupitia wanafunzi wao jijini Dodoma.
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Walimu wakuu shule za Sekondari hapa nchini wametakiwa kuwahimiza wanafunzi wao kushiriki kwa wingi katika mashindano ya Insha inayojumuisha Jumuiya ya wananchama wa SADC na EAC kwani zitawasaidia kuwa wabunifu na kuwajengea uwezo wa kufikiri.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia,William Ole Nasha, wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti kwa washindi wa kitaifa shindano la uandishi wa Insha za Jumuiya SADC na EAC, tukio lililoenda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, na zawadi kwa shule ambazo zimefanya vizuri kupitia wanafunzi wao.
Mhe.Ole Nasha, amesema kuwa ili kuhakikisha mashindano hayo yanashirikisha washindani wengi zaidi ni lazima kuhakikisha wanaoshiriki wanakuwa wengi kwani mashindano hayo yanasaidia Sana hasa katika kuongeza ubunifu, kujiamini na mwanafunzi kutengeneza fulsa mbalimbali.
“Ili tupate washindi wengi katika mashindano haya ni lazima wakuu wa shule za Sekondari wahakikishe wanawahamasisha Sana wanafunzi wengi kushiriki katika mashindano hayo, kwa sababu yanawaongezea fulsa washiriki na kuwasaidia kujiamini Sana”
“Mashindano haya yanawasaidia wanafunzi wetu kuwajengea uwezo wa uandishi, udadisi na kuwa wepesi kufanya tafiti,pia mashindano haya yanasaidia kuwajengea uzalendo pindi wanapokuwa wanawakilisha taifa” amesema Ole Nasha.
Pia amewataka wanafunzi walishiriki na kushinda kuwa Mabalozi wazuri kwa kuhamasisha wenzao nao kuhakikisha wanashiriki mashindano hayo ili kuwa na wawakilishi wengi zaidi katika mashindano hayo na kuwapongeza kwa kushiriki na hatimaye kuibuka washindi wa mashindano hayo.
Amesema mashindano hayo yalianzishwa ikiwa ni sehemu ya mkakati mkubwa wa Jumuiya ya SADC na EAC kujenga uelewa kwa wanafunzi juu kazi na mipango ya Jumuiya hizo kwa wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo ya kuandika insha yenye maada zinazoshabihiana na Jumuiya hizo.
Amesema maada iliyoshindaniwa katika shindano hilo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa “ni kwa namna gani aina mbalimbali za Utamaduni wa watu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaweza kutumiwa kuimarisha utengamano wa kikanda, ukuaji wa uchumi na utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki”.
Wakati kwa upande wa Jumuiya ya SADC ilihusu “ni kwa namna gani mipango inayolenga vijana inachangia katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika ukanda wa SADC”? mada zote mbili zimekuwa Chachu ya mipango ya maendeleo kwa vijana wa Nchi wanachama.
Kwa upande wake mratibu wa tukio hilo na la uandishi wa insha Sylvia Chinguwile, amesema maada za zinazoshindaniwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa Nchi na baadaye Nchi wanachama kuwajibika kutangaza na kubainisha vigezo vya washiriki.
Amesema baada ya kupita katika michakato huo huwasilishwa wizarani na kuteuliwa insha bora katika ngazi ya shule na kusahihishwa na jopo la wataalamu na zile za EAC husimamiwa na balaza la mitihani, na insha tatu bora za SADC hupelekwa Botswana ili kuidhinishwa na mataifa Nchi wanachama, wakati insha tano bora huwasilishwa Arusha Makao makuu ya Jumuiya kushindanishwa na Mataifa mengine.
Amesema kwa upande wa EAC mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza ni Vanessa Lema, kutoka Longido Sekondari kidato Cha sita, wakati wa pili ni Thomas Kalisti, Kibasila Sekondari Dar as saalam kidato Cha Tatu, huku kwa ujumla wake Wakiwa 13.
Nae Kaimu Kamishna wa Elimu hapa nchini Mwalimu Augusta Lupokela, ameipongeza Wizara ya elimu kwa kuweza kuwasimamia mwanzo hadi mwisho wa mashindano hayo amesema kupitia mashindano hayo wameweza kujipambanua kuwa bado elimu yetu ipo katika Hali nzuri ukilinganisha wanavyoiongelea watu wengine.
Wakati mmoja wa wanafunzi ambaye alifanya vizuri katika uandishi wa Insha kwa maada zote Julieth Mpuya, kutoka Kilangalanga Sekondari kidato Cha kwanza, amesema kilichompelekea kufanya vizuri ni ujasili, kujituma kufuatilia maada na kuamini kuwa anaweza na hatimaye kufanya vizuri.