*************************************
Moja ya timu zilizofuzu kwa hatua ya 16 bora ya ligi mabingwa barani Ulaya ni Napoli ya Italia ikishinda bao 4-0 katika mechi yake ya Jana Usiku dhidi ya KRC Genk.
Licha ya mafanikio hayo lakini Napoli wameamua kumtimua kazi kocha wake mkuu Carlo Ancelott ambaye anatajwa huenda akatimkia katika klabu ya Arsenal au Everton.
Napoli licha ya kufanya vyema katika ligi ya mabingwa Ulaya lakini imekua ikifanya vibaya katika ligi kuu nchini Italia huku ikielezwa kwamba hakuna maelewano baina ya bodi na benchi la ufundi.