Home Michezo ARSENAL YAFUTA GUNDU,YAICHAPA 3-1 WEST HAM NA KUSHINDA  MECHI YA KWANZA KATI...

ARSENAL YAFUTA GUNDU,YAICHAPA 3-1 WEST HAM NA KUSHINDA  MECHI YA KWANZA KATI YA 10

0

Nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia bao la tatu dakika ya 69 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham United jana Uwanja wa London, huo ukiwa ushindi wa kwanza katika mechi 10 za Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya Arsenal katika ushindi huo wa kwanza pia kwa Freddie Ljungberg tangu arithi mikoba ya Mfaransa, Unai Emery yalifungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 60 na Nicolas Pepe dakika ya 66,  wakati la West Ham lilifungwa na Angelo Ogbonna dakika ya 38 PICHA ZAIDI SOMA  HAPA