Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara, Edwin
Rutageruka akimkabidhi zawadi ya Mkoba unaotokana na Bidhaa za
ngozi,Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye pia ni
mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho ya Nne ya Viwanda, Bw. Leo
Lyayuka(kulia) mara baada ya kufunga Maonesho hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye
pia ni mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho ya Nne ya Viwanda, Bw. Leo
Lyayuka (wa pili kulia), akimkabidhi cheti cha Ushiriki, Amri Hamza kutoka
kampuni ya Amir Hamza Ltd na Amimza Ltd, mara baada ya kufunga maonesho
hayo leo Desemba 09, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye
pia ni mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho ya Nne ya Viwanda, Bw. Leo
Lyayuka (wa pili kulia), akimkabidhi cheti cha Ushiriki, Meneja Mawasiliano kutoka
Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John, mara baada ya kufunga Maonesho hayo leo
Desemba 09, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye pia
ni mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho ya Nne ya Viwanda, Bw. Leo Lyayuka
(wa pili kulia), akimkabidhi cheti cha Ushiriki, Dochi Serif Kibaraza, kutoka
kiwanda cha Sukari Zanzibar, mara baada ya kufunga Maonesho hayo leo Desemba
09, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi kutoka shule za Jiji la Dar es Salaam, wakionesha
gwaride la kumuongoza mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda kutoka
Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Leo Lyayuka, mara baada ya kuwasili kufunga
maonesho hayo yaliyoanza Desemba 04, 2019 na kuhitimishwa leo Desemba 05,
2019.
Baadhi ya Mshine za kutengeneza Bidhaa mbalimbali kutoka SIDO
zikiwa katika maoenesho ya Nne ya Viwanda na Bidhaa za ndani yaliyoanza
Desemba 04, 2019 na kuhitimishwa leo Desemba 05, 2019 na Mkurugenzi wa
Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Leo Lyayuka.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini (TANTRADE), imetakiwa kufanyia kazi mapendekezo ya kufanyika kwa maonesho ya biashara kwa mwaka ujayo jijini Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamishia makao makuu ya serikali katika jiji hilo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati akihitimisha Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere, Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara nchini Bw. Leo Lyayuka, amesema kuwa TANTRED walifanyie kazi haraka pendekezo hilo na kutoa mrejesho kwa wamiliki wa viwanda nchini ili maandalizi yafanyike haraka.
Aidha Bw.Lyayuka amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kununua na kutumia bidhaa za kitanzania ili kuwahakikishia wazalishaji uhakikika wa soko na kuongeza juhudi ya kuzalisha Zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw.Edwin Rutageruka amesema kuwa wanaandaa kanuni ambazo zitatoa mwongozo wa uratibu wa maonesho hapa nchini kwani hivi sasa kumekuwepo na wimbi la watu kufanya maonesho kama gulio.
Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yalinza tarehe 5 na kuhitimishwa leo tarehe 09 Desemba 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere