Home Michezo KILI STARS YAPINGWA ,ZANZIBAR ANGALAU

KILI STARS YAPINGWA ,ZANZIBAR ANGALAU

0

Na Mwandishi Wetu, 
TANZANIA Bara imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuchapwa 1-0 na Kenya katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda.
Bao lililoizamisha Kilimanjaro Stars inayofundishwa na kocha Juma Mgunda anayesaidiwa na Zubery Katwila limefungwa na Hassan Abdallah dakika ya nne tu akimalizia pasi ya Anthony Wambani aliyewatoka mabeki kiustadi.
Bara itarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Zanzibar kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Sudan Desemba 14, wakati Nusu Fainali zitafuatia Desemba 17 na Fainali Desemba 19.

Mechi nyingine ya CECAFA Challenge kundi hilo , Zanzibar ililazimishwa sare ya 1-1 na Sudan mchana Uwanja wa Lugogo.
Makame Khamis alianza kuwafungia Zanzibar Heroes dakika ya 55, kabla ya Montasir Yahia kuisawazishia Sudan dakika ya 90.
Zanzbar itarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Tanzania Bara kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Kenya Desemba 14.
Kikosi cha Kenya kilikuwa; Samuel Odhiambo, Joash Onyango, Lawrence Juma, Kevin Kimani/Cliffton Miheso dk72, David Owino, Samuel Olwande, Anthony Wambani/ Whyvone Isuza dk82, Oscar Wamalwa, Kenneth Muguna, Johnstone Omorwa na Hassan Abdallah/ Daniel Sakari dk90+3.
Tanzania Bara; Aishi Manula, Mwaita Gereza, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Bakari Mwamnyeto, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Miraj Athumani ‘Madenge’/Hassan Dilunga dk70, Muzamil Yassin, Paul Nonga/ Ditram Nchimbi dk65, Cleophace Mkandala na Lucas Kikoti/Eliuter Mpepo dk43.