Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akiangalia bidhaa zilizobuniwa na wanafunzi na walimu wa chuo cha ufundi VETA wakati alipotembelea katika banda hilokushoto ni Dora Tesha afisa Uhusiano wa VETA na katikati ni Bw. Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Dora Tesha afisa Uhusiano wa VETA alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere Katikati ni Bw. Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kuhusu kiti kilichobuniwa na wanafunzi wa VETA kutoka kwa Dora Tesha afisa Uhusiano wa VETA alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere kulia ni Bw. Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE.
……………………………………………..
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) inayoshiriki kwenye Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere.
Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya ametembelea banda hilo mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ambayo viwanda na wajasiriamali pamoja na taasisi mbalimbali zinaonesha bidhaa zao.
Waziri Manyanya alipata maelezo namna taaisi hiyo ya elimu ya ufundi inavyotolewa na kuwapatia ujuzi vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa katika kuliletea maendeleo taifa kwa teknolojia mbalimbali za kiufundi.
Pamoja na mambo mengine katika maonesho hayo VETA inatoa elimu kwa wananchi juu ya mafunzo yanayotolewa na vyuo vya VETA na kuhamasisha vijana kujiunga na mafunzo hayo ili waweze kujiajiri na kuanzisha viwanda vidogo.
Kupitia maonesho hayo pia washiriki wa VETA wanaonesha ubunifu unaofanywa na walimu na wanafunzi pamoja na kuonesha kazi mbalimbali za wahitimu waliofanikiwa kujiajiri wenyewe.
VETA inaongozwa na kauli mbiu inayosema “Maendeleo Endelevu ya Viwanda Yanahitaji Nguvu Kazi yenye Ujuzi.