Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM. Wengine ni Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM
Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS akizungumza na wageni waalikwa
Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar akipokea picha ya zawadi kwenye mahafali hayo
Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen, Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar.
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Anita Otto Ringia akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU
Mhitimu wa shahada ya Uzamili Beatrice Issara akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wahitimu wenzie kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Pendaeli Mbise akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU
…………………………………………………
Kampuni ya Equinor Tanzania inafuraha kufanya mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliowafadhili kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering and Project Management.
Wahitimu hao wamefadhiliwa kupitia programu ya ufadhili ya Equinor Tanzania, inayofahamika kama ‘Angola Tanzania Higher Education Initiative’ (ANTHEI). Programu hiyo inayosimamiwa na Equinor inatoa ufadhili kamili kwa wanafunzi kumi kila mwaka kusoma Shahada ya Uzamili (MSc) katika masomo ya Petroleum Geoscience and Petroleum Engineering katika Chuo Kikuu cha Norwegian University of Science and Technology (NTNU), ambacho kinafanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Programu hiyo imetengenezwa katika muundo ambao wanafunzi wanasoma mwaka mmoja Norway na mwaka wa mwisho wa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya Equinor, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na NTNU, Programu hiyo ya msaada wa elimu chini ya Equinor, ulianza mwaka 2012 na unafikia mwisho mwaka huu. Jumla ya wahitimu 64 tayari wamefaidika na program hii, kwa na kubahatika kufanya kazi katika vitengo mbalimbali vya serikali pamoja na sekta binafsi.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Makamu wa Rais Mwandamizi ambaye pia ni Meneja Mkazi wa Equinor hapa nchini Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, alisema, “Equinor inafuraha kufanya kazi kwa kushirikiana na vyuo vikuu ili kufikia lengo lake la kujenga uwezo ambalo ni jambo muhimu katika maendeleo ya sekta muhimu ya gesi nchini Tanzania. Lengo letu ni kuona watanzania wanapata mafunzo ili kuwa na sifa stahiki ili kutoa mchango wao katika ukuaji wa sekta hii kwa namna zote, moja kwa moja na isivyo moja kwa moja .”
“Hapa Equinor tunatilia mkazo zaidi katika utendaji endelevu duniani kote. Mbinu ya Equinor ni kujenga mazingira endelevu ya shughuli zetu za msingi na kuchangia maendeleo pasipokuwa na kikomo mahali tunapofanya kazi,” aliongeza kusema Dkt. Mette.
Wakati wa kipindi cha miaka sita ya Equinor kupitia programu yake ya uwezeshaji kumekuwapo na mafanikio ikiwa ni pamoja na maendeleo ya tafiti za Mafuta na Gesi, ambavyo vilipelekea uwepo wa Shahada ya Uzamili katika Fedha na Uhasibu kwenye Mafuta na Gesi (Master for Finance and Accounting in Oil and Gas -MFA-OG) vikitolewa kwa ushirikiano wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Stavanger. Halikadhalika Equinor imetoa msaada wa kiufundi katika Chuo Kikuu cha Barcelona pamoja na kuhakikisha uwepo wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Petroleum Geosciences kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Hii pia ilijumuisha mafunzo wa wakufunzi, ufundishaji kwa njia ya mtandao, na ujenzi wa maabara ya analojia
Katika nyongeza ya ufadhili, mwaka huu Equinor imejenga maabara ya na kutoa mafunzo kwa mtu wa maabara katika Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Uhandisi Dar es Salaam (UDSM), na kuwezesha ufundishaji wa Shahada ya Uzamili katika Uhadisi wa Petroli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.