Washindi wa Tuzo za FISA wakiwa pamoja na menejimenti ya taasisi ya Lambokile wakati wa utangazaji wa msimu mpya wa tuzo kwa vijana katika sekta mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
Mshindi tuzo za FISA msimu uliopita Hellena Sillas akizungumza juu ya fursa na mafanikio aliyoyapata kutoka kwenye kampuni hiyo ambapo amewashauri vijana kutumia fursa za namna hiyo ili waweze kujikomboa na kuikomboa jamii kwa ujumla, Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Lambokile, Lawrence Ambokile akizungumza wakati wa kutangaza msimu mpya wa tuzo za FISA ambapo ameeleza kuwa vijana wengi waliopita katika taasisi hiyo wamekuwa mabalozi wazuri, hivyo ni vyema vijana wakatumia fursa hiyo, Leo jijini Dar es Salaam.
***********************************
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira ; Anthony Mavunde anategemewa kutoa tuzo 20 kwa vijana walioleta matokeo chanya katika jamii kupitia miradi wanayoifanya na hiyo ni pamoja na kuwapatia msaada wa karibu ili kuongeza wigo wa huduma zenye matokeo chanya kwa jamii na hiyo ni pamoja na kuwapatia misaada ya karibu ili waweze kufikia malengo yao na kuwa mfano na mabalozi bora kwa jamii mzima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa taasisi ya Lambokile ambayo imeandaa tuzo hizo Lawrence Ambokile amesema tuzo zitatolewa Desemba 21 na hilo litaenda sambamba na kongamano la vijana.
“Waziri Mavunde atatoa tuzo hizo tarehe tajwa katika ukumbi wa Mlimani City kabla yake yaani tarehe 20 vijana watakutana na wadau wa maendeleo na kujadili changamoto na fursa za zilizopo na zijazo katika ubunifu katika kuelekea uchumi wa viwanda” Ameeleza.
Ambokile amesema kuwa malengo ya kutoa tuzo hizo zilizoanza kutolewa mwaka 2018 yalijikita katika kuwatambua vijana wanaoleta matokeo chanya katika jamii kupitia miradi yao.
“The Future I Want Awards (FISA) ilianzishwa na vijana ikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi na sio kutegemea ajira pekee, na kupitia tuzo hizi vijana wenye ndoto na malengo wanakaribishwa kushiriki ili tujenge taifa imara” Ameeleza.
Kuhusiana na mchakato wa ushiriki na vigezo Ambokile amesema;
“Fomu za maombi zinapatika kwenye tofuti ya taasisi hiyo mitandao ya kijamii na kutokana na mahitaji kuwa mengi wameongeza siku tano za kuchukua fomu hizo kuanzia leo na walengwa ni vijana kuanzia miaka 15 hadi 35 ambao wanaweza kujipendekeza au kupendekezwa kabla ya majaji kupitia na hatimaye kupata washindi katika tuzo zote zitakazotolewa” ameeleza.
Mbali na kupewa tuzo hizo ambapo kila tuzo ina thamani ya shilingi milioni moja washindi watapata fursa ya kupata ushauri wa kibiashara, kupata mitaji pamoja na kuunganishwa na wadau mbalimbali wa kimaendeleo.
Baadhi ya washiriki wameeleza mafanikio waliyoyapata baada ya kuwania na kushinda tuzo ambapo wameeleza mahitaji na changamoto za kijamii wamezichukua Kama fursa na hiyo ni pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimaendeleo katika kuwawezesha vijana wengine.