Home Mchanganyiko RC MAKONDA ATOA OFA YA UKAGUZI NA MATENGENEZO YA MAGARI YA WANANCHI...

RC MAKONDA ATOA OFA YA UKAGUZI NA MATENGENEZO YA MAGARI YA WANANCHI BURE KWA MUDA WA SIKU TANO KWENYE GARAGE ZA KISASA ZAIDI YA 100 ZILIZOMUUNGA MKONO.

0

**********************************

Katika kuelekea Msimu wa Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ofa kabambe kwa wananchi wote wenye magari kufanyiwa ukaguzi wa magari yao na kupatiwa ushauri wa kitaalamu bure kwa muda wa siku tano kuanzia Jumanne ya Disemba 10 hadi 15 kwenye zaidi ya Garage100 zilizopo jijini humo.

RC Makonda amesema lengo la kutoa ofa hiyo ni kuwawezesha wananchi wanaopenda kusafiri na familia zao kula sikukuu kusafiri salama na kurudi salaam wakiwa na uhakika na usalama wa vyombo vyao vya usafiri ili kuepusha ajali zitokanazo na ubovu wa magari.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kufanya kikao na Wamiliki wa Garage na mafundi na kuwapa ombi la kumsaidia kufanya ukaguzi wa magari ambapo wamiliki hao wamepokea kwa mikono miwili ombi hilo la Mkuu wa Mkoa kwakuwa linalenga kuepusha ajali.

Aidha RC Makonda amesema licha ya zoezi hilo kuwasaidia wananchi pia litawafanya wenye Garage kujitangaza na kuongeza idadi ya wateja wapya.

Hata hivyo RC Makonda ameeleza mpango wa kuwaunganisha watu wa Garage na Chuo cha ufundi Stadi VETA ili watoe mafunzo na vyeti jambo litakalowafanya kuongeza ujuzi na Maarifa ya kazi na kujenga imani kwa wateja huku akiwahimiza wenye Garage kuzirasimisha Garage zao ili waweze kulipa kodi serikalini na kutambulika.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kuwa majina ya Garage zitakazotoa huduma hiyo zitatangazwa kwenye vyombo vya habari siku yoyote kuanzia leo ili Mwananchi achague wapi Kwa kupeleka Gari lake.