Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali wakiwasili ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Glonency Mkoani Morogoro tarehe 4 Disemba, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Loata Ole Sanare.
Baadhi ya Manaibu Waziri na Mawaziri wa Wizara walioshiriki katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji wakiwasikiliza wachangiaji mbalimbali walioalikwa katika mkutanouliolenga kusikiliza changamoto za Wafanyabiashra uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro tarehe 4 Disemba, 2019.
Baadhi ya Manaibu Waziri na Mawaziri wa Wizara walioshiriki katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji wakiwasikiliza wachangiaji mbalimbali walioalikwa katika mkutanouliolenga kusikiliza changamoto za Wafanyabiashra uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro tarehe 12 Disemba, 2019.
Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuingia ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
………………………………………………
Na Farida Saidy,Morogoro
Wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika mkutano wa Mashauriano ulioongozwa na Mawaziri zaidi ya 10 kutoka wizara Mbalimbali mkoani Morogoro, wameeleza kuwa kinacho wakwamisha katika shughuli zao ni Utitili wa Kodi unaosababishwa na Mfuno usio rafiki kwa taasisi za serikali zilizopewa jukumu la ukusanyaji wa Kodi.
Hoja za wafanyabiashara na wawekezaji zinakuja ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano ya Mashauriano ikihusisha wizara mbalimbali, mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Morogoro,Viongozi wa serikali kutoka wizara mbalimbali na watendaji ngazi za mikoa wilaya na Halmashauri.
Wanasema pamoja na dhamira ya serikali kutaka kufikia uchuni wa kati kwa uwekezaji wa viwanda, kinacho wakwamisha kuendana na sera hiyo ni mfumo wa Kodi unaowafanya kushindwa kuendana malengo yao.
Awali kabla ya hoja hizo, viongozi wa serikali mkoani hapa wamesema dhamira ya kikao hicho ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji, kuweka bayana changamoto zao ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Msimamo wa serikali ni kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, kuendana na sera ya serikali kufikia nchi yenye uchumi wa kati.
Zaidi ya wafanyabiasha na wawekezaji 500 kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa huu wamehudhuria kikao hicho cha mashauriano ambapo pamoja na mambo mengine kimelenga kuimarisha uhusiano baina yao na serikali ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo 2020-2025.