Baba Askofu Mstaafu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila ambaye atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Jumatatu Desemba 9, 2019 .
Bishop Flaston Ndabila (kulia) na Mke wake Janeth Ndabila wa Kanisa la ABC Tabata waandaaji wa maadhimisho hayo wakiwa katika picha ya pamoja. Maadhimisho hayo yatakwenda sanjari na kuwapongeza wanandoa hao kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa, miaka 25 ya huduma na miaka 50 ya kuzaliwa.
Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya)
Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini).
Pastor Fred Msungu.
Pastor Hererimana Tharcise (Burundi)
Bishop Robson Simkoko kutoka Malawi.
Apostle Moses Silwamba (Zambia)
Na Dotto Mwaibale.
MAASKOFU na wachungaji kushiriki maadhimisho ya miaka 25 ya huduma ya Abundat Blessing Centre ( ABC) yatakayofanyika Jumatatu Desemba 9, 2019 .
Maadhimisho hayo yatakwenda sanjari na Kongamano na Tamasha la jimbo za Injili ambayo yatafanyika katika Kanisa la ABC lililopo Tabata Mandela jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa maadhimisho hayo , Askofu Flaston Ndabila ambaye ni kiongozi mkuu wa kanisa hilo, alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa siku ya hitimisho ambayo itakuwa ni Desemba 9 mgeni rasmi atakuwa ni Baba Askofu mstaafu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dkt. Asumwisye Mwaisabila
mwenye kalama kubwa ya uneneji.
“Maadhimisho hayo yatakuwa na kongamano ya vijana, wanandoa na sherehe tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 200, maaskofu na wachungaji kutoka ndani na nje ya nchi” alisema Ndabila.
Alisema kongamano la vijana litakuwa la siku moja ya Desema 6 na litafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 jioni na tamasha la uimbaji walengwa ni vijana kutoka vyuo vikuu na makanisa mbalimbali.
Askofu Ndabila aliongeza kuwa Desemba 7 kutakuwa na kongamano maalumu la ndoa na familia ambalo litahusisha maaskofu na wachungaji hao.
Aliwataja baadhi ya watumishi wa mungu watakaohudhuria maadhimisho hayo ambapo pia kutakuwa na kumpongeza Askofu Ndabila kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa yake na miaka 50 ya kuzaliwa kuwa ni Bishop Robson Simkoko kutoka Malawi, Mchungaji Moses Silwamba (Zambia), Pastor Hererimana Tharcise (Burundi) Pastor Fred Msungu na muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Arusha, Eliya Mwantondo.
Wengine ni Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya) na Bishop Musa Ngobese (Afrika Kusini).
Kwa mawalisiano zaidi kuhusu maadhimisho hayo piga simu namba 0754762301 na 0715684590.