MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha kawaida cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar,kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid,kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.
***********************************
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo Disemba 05, mwaka 2019 ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 4:00 Asubuhi.
Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.
Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 (2).
Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM.
Viongozi mbali mbali wameudhuria Kikao hicho wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.