Na innocent Natai, Morogoro
Mahakama ya Wilaya ya Ifakara Mkoani Morogoro imemuhukumu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi Milioni Mbili pamoja na kuviteketeza viuatilifu kwa gharama zake mwenyewe, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yerusalem Mwamaja miaka 49 (Mhehe) baada ya kupatikana na hatia ya kupatikana na viuatiliafu visivyo sajiliwa
Hukumu hiyo imetolewa Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Binge Njaga Mashabara, baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi watatu wa upande mshtaka, bila kuacha shaka yeyote.
Hakimu Mashabara alisema vitendo kama hivyo vinawasababishia hasara wakulima na seikali kwa ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa mazingira na kwa Afya za binadamu wanyama na mimea. Hivyo alitoa adhabu hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Awali, Wakili wa Serikali, alidai kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshatakiwa na hivyo kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Katika utetezi wake Yerusalem Mwamaja alikubali mashtaka na aliomba apunguziwe adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho na hata rudia.
Akizungumzia hukumu hiyo baada ya kutoka Mahakamani hapo Bw Solomon Shedrack Mungure amabaye ni Mkurugenzi wa Viuatilifu kutoka ofisi ya TPRI Dar es Saalam ameipongeza Mahakama hiyo kwa adahabu iliyotoa kwani itakuwa ni fundisho kwa wengine wenye tabia za kufanya biashara za viuatilifu visivyo Sajiliwa.
Aidha ametoa rahi kwa wauzaji na wasambazaji wa Viuatilifu nchi nzima wenye tabia za kuuza na kusambaza viuatilifu visivyo sajiliwa na kukaguliwa na TPRI kuacha mara moja kwani zoezi la ukaguzi na kuwabaini watu kama hao halikomi ni la kila siku na kila saa hivyo watakamatwa mara moja na kuwafikisha mahakamani.
Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa kuuza au kusambaza viuatilifu bila kwa na elimu pia ni kosa kwani kunaweza kumsababishia madhara msambazaji au muuzaji wakati wa ufanyaji biashara bila kuwa na elimu ya namna bora na salama ya kufanya biahara hiyo, hivyo ni vyema wasio na taaluma hiyo kuacha kufanya biashara hizo mara moja na wafuate kanuni na taratibu za kupata mafunzo na kibali cha kufanya biashara hizo.