Home Mchanganyiko WAZIRI BASHUNGWA KUKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA VIWANDA VYA NGOZI NA...

WAZIRI BASHUNGWA KUKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA VIWANDA VYA NGOZI NA NYAMA DESEMBA 5 MWAKA HUU

0

*******************************

Wizara ya Viwanda na Biashara inapenda kuwafahamisha wenye
Viwanda vya Nyama, Ngozi pamoja na wadau wote wa sekta hiyo kuwa
Mhe.Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara anatarajia
kukutana na wadau wa sekta hiyo Alhamis tarehe 05 Desemba, 2019,
kuanzia saa 5.30 asubuhi katika ukumbi wa Mikutano uliopo ofisi za
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Madhumuni ya mkutano ni kujadili mikakati mbalimbali ya Serikali
inayowekwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo na wadau husika. Kwa
Maelezo zaidi wasiliana na Wizara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
kwa Umma.