Home Mchanganyiko Tanzania kuimarisha, kuendeleza ushirikiano na Falme za Kiarabu (UAE)

Tanzania kuimarisha, kuendeleza ushirikiano na Falme za Kiarabu (UAE)

0

Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Mhe. Khalifa
Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akihotubia wageni waalikwa katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mhe. Balozi, Khalifa
Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) mara baada ya kumaliza kuhutubia wageni waalikwa katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wageni waalikwa wakiimba nyimbo za taifa za Tanzania pamoja na ya Falme za Kiarabu (UAE) kabla ya kuanza rasmi kwa maadhimisho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

**********************************************

Serikali ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano wake na Falme za Kiarabu (UAE) katika sekta za biashara, miradi ya maendeleo, utalii, utamaduni, usafirishaji, kilimo na afya.

Akiongea katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ili kukuza na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ni muhimu pia kupanua maeneo ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili hyaakiwemo ya utalii, kilimo na miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tayari tumeanza maandalizi ya mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) ambao utafanyika hapa nchini Tanzania mwaka 2020, baada ya mkutano wa kwanza wa JPC ambao ulifanyika Desemba 2016 Abu Dhabi wakati ambao, makubaliano hayo yalipo sainiwa”. Amesema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi aliongeza kuwa, makubaliano hayo yaliyosainiwa Abu Dhabi ni pamoja na Mkataba wa Huduma za Hewa za Kigeni (BASA) na Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Utalii. Tunatarajia kupanua wigo wa ushirikiano wetu katika mkutano ujao wa JPC.

Kama moja ya Makati wa uwekezaji, tuko tayari kuhakikisha kuwa wawekezaji
wanawekeza Tanzania. Aidha, mbali na maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania (Blue Print)yaliyoanza Julai, 2019, tunafanya mashauriano ya ndani mkataba wa kuepusha na na tozo za ushuru mara mbili; na makubaliano ya mkataba wa pamoja juu ya kukuza na kuendeleza ulinzi wa uwekezaji aambapo kwa makubaliano haya ni chanzo cha Falme za Kiarabu (UAE) kuwekeza Tanzania.

 

“UAE imekuwa ikisaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kusaidia juhudi za Tanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile ufadhili wa ujenzi wa barabara kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (ADFD). Ni matumaini yangu kuwa Mfuko utaendeleza usaidizi na kuelekeza miradi mingine ya maendeleo”. Amesema Prof. Kabudi.

 

Kwa upande wake, Kwa upande wake, Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu kwa
nchini Tanzania, Balozi, Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi amesema kuwa Falme za Kiarabu zitaendeleza ushirikiano baina yake na Tanzania kindugu, kidiplomasia, kiuchumi na kuhakikisha kuwa ni wa kudumu.

 

“Napenda kuwafahamisha kuwa Falme za Kiarabu (UAE) utaendelea kuwekeza hapa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya kukuza uchumi. Tutaendelea kuwaeleza wawekezaji fursa zilizopo Tanzania ili waendelee kuja kuwekeza”. Amesema Balozi, Mohamed Al- Marzooqi.