Home Mchanganyiko RAIS WA TCCIA BW. PAUL KOYI AZINDUA TOVUTI YA LAKE VICTORIA BASIN...

RAIS WA TCCIA BW. PAUL KOYI AZINDUA TOVUTI YA LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019 LEO

0

Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) akizindua tovuti maalum ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019. ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili kulia kwa ke ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha na Bw. Gabriel Nderumaki Mkuu wa Chaneli ya Safari inayoonesha masuala ya utalii.

Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti maalum ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019. ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha na kushoto ni Franklin Mziray Mshauri wa masuala ya habari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha akizungumza katika uzinduzi hio katikati ni Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na kulia ni Bw. Gabriel Nderumaki Mkuu wa Chaneli ya Safari inayoonesha masuala ya utalii.

Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashashamara baada ya kufanya uzinduzi huo.

Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Ali Nchahaga mratibu wa maonesho.

………………………………………………………….

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TA L-VIC INVESTMENTS LIMITED Bw. Anic Kashasha amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufungua uchumi wa utalii katika mikoa  ya Kanda ya Ziwa, kufuatia kuyapandisha hadhi mapori kadhaa ya akiba na kuyafanya hifadhi za Taifa (National Parks) ambazo sasa zitaruhusu shughuli za uchumi wa utalii kushamiri katika mikoa hiyo

Bw Kashasha amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Cortyad Oysterbay jijini Dar es salaam wakati akizungumzia Uzinduzi wa tovuti ya LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019  ambayo itatumika kwa ajili ya washiriki wa maonesho hayo kujisajili.

amesema ili kuunga mkono juhudi za  Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika kukuza utalii kanda ya ziwa tumeanzisha  tovuti rasmi ambayo itatumika kwa wadau kujiorodhesha kwa njia ya mtandao ili kushiriki kwenye maonyesho ya utalii yatakayofanyika Kabuhara Beach, Maruku, Bukoba Vijijini mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Disemba hadi 30  2019, ambapo pia watahudhuria kwenye Kongamano la Utalii litakalofanyika tarehe 28 na 29 Disemba 2019 kwenye Ukumbi wa ELCT Hotel Bukoba mjini. 

Kashasha amemshukuru  pia Bw. Paul Koyi, Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kwa kutenga muda wake pamoja na majukumu yake mengi na kujumuika  kwake katika uzinduzi wa tovuti hiyo.

Huu ni uthibitisho wa utayari wa uongozi mpya wa TCCIA chini ya uongozi wake, kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa karibu zaidi na wafanyabiashara ili kuongeza ufanisi katika shughli za biashara.

Ni muhimu sana kuliweka wazi hili kwamba Bw. Paul Koyi, Rais wa TCCIA mwenyewe akiwa ni mfanyabiashara mzoefu ni mwenye maono ya kibiashara kweli. Ninalisema hili kwa sababu tulipokutana naye na kumuelezea ni nini tunachokifanya, alituelewa haraka sana na kuahidi kutupatia ushirikiano ili kuhakikisha malengo ya mradi wa Lake Victoria Basin Tourism Expo yanafanikiwa.

Aidha, alikubali mara moja kupokea ombi letu la kushirikiana pamoja na TCCIA kwenye mradi wa muda wa kati ambapo tutajikita katika kufanya shughuli za kusisimua utalii wa ndani na utalii wa kikanda (Intra-EAC Tourism).

Ameongeza kuwa jambo hili linatarajiwa kufanyika kwa kuitumia rasilimali kubwa ya maji ya Ziwa Viktoria ambapo Bonde lake ni mali ya asili inayomilikiwa na nchi 5 kati ya 6 zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkakati huu utatekelezwa kwa kuishirikisha kampuni ya Marine Services Company Limited (MSCL), inayomiliki meli na kuendesha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwa na meli 15 ambapo meli 9 kati ya hizo zimo na zinafanya kazi ndani ya Ziwa Viktoria.  

Hivyo tunatarajia kuwekeana saini makubaliano ya kushirikiana (MOU) na Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) ambayo itatuongoza kuingia kwenye ushirikiano wa kufanya kazi pamoja na East African Business Council (EABC) kwenye mradi wa kusisimua na kukuza utalii wa kikanda (Intra-EAC Tourism).

Amesema kuwa wameshaanzisha mchakato wa kuzishirikisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Maliasili  na Utalii, Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi yake ya Lake Victoria Basin Commission, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na TradeMark East Africa.

Amemaliza  na kusema mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa kukuza utalii lakini pia kuongeza kasi ya mashirikiano baina ya wananchi wa nchi wana chama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.