Injinia Julius Enock kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa CCEMI jijini Dar es Salaam na yameandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sehemu ya Washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo yalioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mtaalamu mwelekezi wa mpango wa kupunguza Matumizi ya kemikali jamii ya hydrochlofluocar- cons(HCFCs) kemikali zinazotumika kweny viyoyozi na majokofu, Bwana Marvin Kamurthuzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP) akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa
na Ofisi ya Makamu wa Rais.