Home Mchanganyiko Wataalam ufundi vifaa tiba wajengewa uwezo Mloganzila

Wataalam ufundi vifaa tiba wajengewa uwezo Mloganzila

0

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Grace Magembe akizungumza wakati wakufunga mafunzo ya ufundi vifaa tiba yaliyofanyika katika hospitali ya Mloganzila, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa KOFIH, Bi. Park Bokyung.

Baadhi ya wataalam wa ufundi vifaa tiba kutoka mikoa mbalimbali nchini
wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa kufunga
mafunzo hayo.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Magembe na
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila Dkt. Magandi wakiwa katika
picha ya pamoja na wataalam hao mara baada ya kufunga mafunzo hayo.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi
akiwapongeza wataalam wa ufundi vifaa tiba waliomaliza mafunzo ya mwezi
mmoja hospitalini

.************************************

Wataalam ufundi vifaa tiba wamepatiwa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo wakufanya matengenezo ya mashine mbalimbali zinazotumika katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili-Mloganzila, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Grace Magembe amewataka
wataalam hao kuwajengea uwezo wataalam wengine ili kuongeza ufanisi kazini.

“Hakikisheni mnaacha alama kwa kuwajengea uwezo wataalam wengine ambao
hawakupata fursa ya kushiriki katika mafunzo haya ili kuongeza idadi ya wataalam wa ufundi vifaa tiba nchini,” amesema Dkt. Magembe.

Dkt. Magembe amewashukuru Korea Foundation for International Healthcare
(KOFIH) kwa kushirikiana kaika kuandaa mafunzo hayo na kueleza kuwa serikali
itaendelea kushirikiana nao kwa faida ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth
Magandi amesema kutolewa kwa mafunzo hayo kutaendelea kuwapa ujuzi katika kufanya matengenezo ya vifaa tiba kwa wakati ili kuwawezesha watoa huduma za afya kutoa huduma pasipo shida yoyote.

Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa mwezi mmoja na kushirikisha wataalam kutoka Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Lindi, Tanga, Geita, Mwanza, Arusha, Pwani, Mtwara, Singida, Mbeya, Kilimanjaro, Shinyanga na Katavi.