Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa pili kulia) akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi (kushoto) pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wengine katika picha ni Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa na kutambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi akitoa salamu kwa mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akitoa salamu za ESRF kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mkuu wa Ukuaji wa Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla akitoa salamu za UNDP kwa niaba ya Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini Tanzania.Bi. Christne Musisi wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akikabidhi Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa tayari kuzinduliwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi sambamba na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (katikati) akionyesha nakala za Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuzindua rasmi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Mkuu wa Ukuaji wa Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) – Utalii na Huduma za Biashara Bw. Imani Nkuwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mtafiti mshiriki kutoka ESRF Musa Martine wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mwekezaji wa hoteli za fukwe za bahari mkoani Lindi Bw. Sultan Ahmed kutoka Kilwa akitoa ushuhuda kuhusu fursa zilizopo ndani ya mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya za Lindi na Wilaya za Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliowekeza kwenye mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau kutoka ESRF, UNDP, Equinor, Shell, taasisi mbalimbali za serikali na sekta binfasi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MKOA wa Lindi umezindua Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo ambao umeanisha fursa za uwekezaji zilizopo Lindi ili kuvutia wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa na kuimarisha pato la mtu mmoja mmoja na taifa. Mwongozo huo umezinduliwa tarehe 27 Novemba 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.
Mwongozo huo umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na wataalam wa Mkoa wa Lindi chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akizindua mwongozo huo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alitaka fursa hizo zilioanishwa kutekelezwa kimkakati ili kuongeza kipato cha wananchi na Mkoa wa Lindi.
Alisema mkoa wa Lindi umefanyakazi kubwa ya kuongeza kilimo cha korosho na ufuta na kusema hiyo ni fursa kubwa kama ilivyo katika utalii kutokana na kuwa na misitu mingi ya hifadhi na fukwe nzuri zaidi za kitalii nchini na duniani. Alisema inawezekana pia kuanzisha siku maalum ya kula nyama pori wilayani Kilwa ili kuchochea utalii.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi M kuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Machi mwaka huu limeleta wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Alisema Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam ni kati ya taasisi zilizoonesha nia ya kuwekeza na kimepewa ekari 150 za ardhi bure kwa ajili ya Chuo cha Kujenga Boti na Meli. Mwekezaji mwingine ni Sarah Masasi anayetaka kujenga Kiwanda cha kubangua korosho na amepatiwa ekari 50 bure za ujenzi huo.
Alisema kampuni ya kimataifa ya Norway inatarajia kuwekeza kituo cha sayansi, ufugaji na kilimo na kampuni kutoka India kuwekeza kwenye uvuvi. Hakutaja majina ya kampuni. Aidha kampuni kutoka Ujerumani, Filloship inafanya mazungumzo kuwekeza mkoani hapa.
Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, kampuni za mafuta na gesi za Equinor, Shell, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa, taasisi za umma, wawekezaji na sekta binafsi, Zambi alisema kutokana na kongamano hilo walianzisha ofisi ya uratibu wa uwekezaji.
”Tunaishukuru TSN (wachapishaji wa magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo) kutufungulia mlango kupata wawekezaji Marekani, Ujerumani, India na nchini,” alisema Zambi. Pia, aliwashukuru Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Lindi.
Alisema kuna miradi mikubwa ambayo inashughulikiwa na serikali kuu hapa mkoani ikiwa ni pamoja na mradi wa kiwanda cha mbolea Kilwa. Mkoa una fursa ya kuwa na kiwanda cha usindikaji chumvi, utengenezaji wa mvinyo kw akutumia korosho, viwanda vya vifungashio, viwatilifu, kubangua korosho na usindikaji wa mafuta ya nazi, alizeti, nishati mbadala nk.
Aidha alisema kwamba fursa katika ngazi ya halmashauri ni pamoja na makundi madogo ya wachambuaji korosho, misitu na utalii na pia kuongeza mnyororo wa thamani katika bidhaa mbalimbali za Kilimo katika ngazi za wilaya na halmashauri.
Alisema kuna utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni na wanamatarajio taaaisi za kitaifa kama Tawa zitasaidia kuwepo na utalii unaowezesha kuchangia kwa kiasi kikubwa pato.
Katika masuala ya uwekezaji katika utalii, mmoja wa wafanyabiashara mkoani Lindi, Sultani Ahmed Sultani alizungumzia kwa kina katika mada yake namna bora ya kuwezesha sekta ya utalii akitaka sekta binafsi kuwezeshwa ili kushiriki katika nafasi hiyo.
Alisema Lindi ina nafasi kubwa ya kuleta watalii kutoka kaskazini na Kusini mwa Afrika kupitia mpango maalumu unaoweza kuungwa na Zanzibar na matunda yake yataonekana.
Dkt. Hoseana Lunogelo, Mtafiti Mwandamizi akizungumzia Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Lindi kwa niaba ya Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), alisema watafiti wake wameona fursa nyingi sana na ziko katika sekta na ngazi zote.
“Kwa hapa Lindi fursa kubwa ipo kwenye mnyororo wa thamani wa zao la Korosho, utalii na madini bila kuisahau gesi. Pia kuna fursa nyingi katika Sekta ya Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Miundombinu na Huduma. “ alisema Dk Kida katika hotuba yake iliyosomwa na Dkt. Lunogelo.
Alisema fursa hizo zilizoainishwa katika mwongozo zikitumika vizuri zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.
Mpaka sasa ESRF imesaidia Mikoa 24 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 14 imekamilisha na Mikoa 10 iko katika hatua mbalimbali. ESRF tayari imeanza kusaidia zoezi hili katika mikoa iliyobaki.
Naye Bw. Ernest Salla akitoa neno kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Christine Musisi ameisihi mikoa iliyokwisha tengenezewa miongozo kuhakikisha kwamba wanafanyaia kazi miongozo hiyo ili kuleta tija.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. Ernest Salla alisema kwamba baada ya kuzinduliwa kwa amwongozo ipo haja kwa mkoa wa Lindi sasa kuangalia vipaumbele na kuchambua vilivyotayari ili kuyafanyiakazi kwa haraka.
Aidha hatua nyingine ya pili ni kutangaza fursa zilizopo na kuandaa mikutano ya uwekezaji kwa kuwakutanisha wawekezaji. Pia watumishi wanaoshughulikia uwekezaji ni vyema wakaandaliwa kusaidia kusukuma mbele gurudumu hilo na kutayarisha nyaraka mbalimbali kielektroniki ili kila mmoja aweze kuzipata.
Pia aligusia haja ya kuhakikisha fursa hizo zinatambuliwa kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na mabalozi wetu nje ili kuuza fursa hizo na kutafuta mitaji ili kuiwezesha sekta binafsi inashiriki kikamilifu.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na ESRF katika kuhakikisha kwamba wanakamilisha kutengeneza Miongozi kwa mikoa iliyobaki.