Timu ya Yanga imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na KMC mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana kutokana na kucheza mchezo wa kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambayo yaliweza kuzaa matunda kwa kila upande Yanga walianza kufumania nyavu dakika ya 73 bao likifungwa na Mrisho Ngasa akimalizia pasi ya Patrick Sibomana.
Dakika ya 90 + 3 walipata Penalti baada ya Kelvin Yondani kumchezea rafu Hassan Kabunda na Kiungo Abdul Hilaly alifunga penalti hiyo .
Hii ni mara ya kwanza kwa KMC kugawana pointi mbele ya Yanga kwani msimu uliopita ilifungwa nje ndani na kuacha pointi sita kwa Yanga kwenye mechi zilizochezwa uwanja wa Taifa.