Home Mchanganyiko TBL YATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA MWAJIRI BORA NCHINI TENA

TBL YATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA MWAJIRI BORA NCHINI TENA

0

Cheti cha Top Employer Award in Tanzania ambacho kampuni imetunukiwa

Wafanyakazi wa TBL wakifurahia Tuzo ya Kampuni muda mfupi baada ya kukabidhiwa 

………………..

Taasisi ya kimataifa ya masuala ya Raslimali Watu na ajira ijulikanayo kama Top Employer Institute, yenye Makao yake makuu nchini Uholanzi imeitunukia tuzo ya Mwajiri Bora 2019  kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), kutokana na kuzingatia na kutekeleza kanuni za Raslimali Watu na uajiri ipasavyo ikiwa ni ushindi wa mwaka wa tatu mfululizo ambapo mwaka juzi na mwaka jana pia ilishinda tuzo hiyo.

Vigezo vya ushindi vimetokana na utafiti wa taasisi ya Top Employers kwa makampuni mbalimbali makubwa nchini ambao ulilenga kwenye utekelezaji kanuni za ajira na Raslimali watu, kampuni ya TBL, imebainika kuwa na vigezo vya ubora katika utekelezaji wa kanuni za ajira zinavyotakiwa. 

Baadhi ya vigezo ambavyo vilifuatiliwa katika utafiti huo kutoka kwa waajiri ni mikakati ya kukuza vipaji vya wafanyakazi, mpangilio wa kazi wa kila siku, mazingira ya kazi, uendelezaji wafanyakazi kimafunzo, utawala sehemu za kazi, taaluma na upandishaji wa vyeo kwa wafanyakazi, maslahi ya wafanyakazi na malipo ya stahiki zao kwa ujumla na desturi ya kampuni.

Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman  alisema “Kampuni yetu inajivunia kupata tuzo hii kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo, hii inadhihirisha mwendelezo wa dhamira yetu wa kuifanya kampuni yetu mwajiri bora anayekidhi viwango vya ndani na vya kimataifa,”

TBL, mbali na kushinda tuzo hii ya uajiri bora ngazi ya kimataifa pia inashikilia rekodi ya kuwa mwajiri bora nchini ambapo mwaka 2015 na 2016 ilishinda tuzo ya Mwajiri Bora inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE). “Tunajivunia kwa mafanikio ya kampuni inayoendelea kuyapata na tutazidi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wetu kwa kuwa ni moja ya sera yetu”. Alisema Redman.

TBL, ilitangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo hii katika hafla iliyofanyika Johanesburg nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni.