Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN UZINDUZI WA BOTI YA UVUVI YA SEHEWA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN UZINDUZI WA BOTI YA UVUVI YA SEHEWA

0

BOTI Mpya ya ya Uvuvi ya Sehewa ikiwa katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria kuizindua Boti Mpya ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Kilimmo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar.Dkt. Makame Ali Ussi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Nahodha wa Biti ya Uvuvi ya Sehewa Ndg. Rashid Abdalla Rashid, akiada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ufukwe  wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza MKURUGENZI Mtendaji Kampuni ya Uvuvi ya Zanzibar (ZAFICO) Ndg.Zahor Kassim Mohamed, wakati akitembelea Boti hiyo ya Sehewa baada ya kuizindua leo katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar.Ndg. Mussa Aboud Jumbe, akionesha aina ya samaki watakaovuliwa na Boti hiyo ya Kisasa ya Uvuvi ya Sehewa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo, 2-12-2019. Katika ufukwe wa bahari ya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)