Mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi.Vumilia Nyamoga,akitoa taarifa kwa Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,alipokuwa na ziara ya kukagua na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa maji Chamwino ( unaohudumia Kata za Msanga,Buigirii na Chamwino)
Kaimu Mkurugenzi na Meneja wa Ufundi Duwasa Mhandisi Kashilimu Mayunga,akimuonesha ramani ya mradi wa maji Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,unajengwa kwa ajili ya kusambaza maji Chamwino.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,akiangalia mchoro unaonesha usambazaji wa maji katika mradi unaojengwa Chamwino alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Chamwino.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji kata ya Msanga wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Tanki la Maji ambalo limejengwa miaka kumi iliyopita lakini halisambazi Maji kwa wananchi wa Kata ya Msanga kutokana na ukosefu wa Umeme.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,akitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi.Vumilia Nyamoga,mara baada ya kukagua na kujionea mradi wa maji katika Kata ya Msanga.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumaliza ziara ya kukagua na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Chamwino (unaohudumia Kata za Msanga,Buigiri na Chamwino)
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………..
Na.Alex Sonna,CHAMWINO
WAZIRI wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amesema wizara itatoa vibali vya kujenga miradi ya maji ambayo wataalam wake hawana uwezo wa kujenga na si vinginevyo.
Pro.Mbarawa ametoa kauli hiyo leo katika ziara yake wilaya ya Chamwino ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji.
Amesema kwasasa wizara imefuta utaratibu wa kutangaza zabuni kwa ajili ya kuwapata wakandarasi kwa kuwa utaratibu huo unachelewesha miradi na kusababisha gharama kubwa ikilinganishwa na wizara kutumia watalaamu wake.
“Hizi kazi za kuchimba mitalo, kujenga tenki la maji la lita milioni mbili, kuchimba visima tuna uwezo kubwa tuna wataalam wazuri kushinda hata hao wakandarasi, naomba nyie wahandisi muelewe na pale mkileta vibali vya kusaini kwa ajili ya wakandarasi kujenga miradi hiyo mimi si saini,”amesema.
Amebainisha kuwa kwasasa kuna miradi 40 ambayo inatekelezwa kwa kutumia ‘force account’ na wamepata faida kubwa.
“Mfano kuna mradi wa maji ulikuwa ujengwe kule Nkasi Kilando Sh.Bilioni 4.6 lakini tumejenga kwa Sh.Bilioni 3.2, hata Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) wakileta gharama kubwa nawaondoa siwapi kazi, hatutaki nao wawe na gharama kubwa,”amesema.
Waziri Mbarawa amesema kuna miradi ambayo wataalam wa wizara wana uwezo mkubwa wa kufanya na kwamba lazima wajengeane uwezo wa kazi.
“Miaka yote tumekaa hii Wizara hatujengi uwezo hata kubadilisha nati anaitwa mkandarasi, wakati nyumbani kwako ukitaka kubadili nati unafanya mwenyewe, najua wakandarasi wanapiga vita utaratibu huu, lakini niwaambie serikali imeamua kutumia utaratibu huu,”amesema.
Amesisitiza ataendelea kuwatoa kwenye nafasi wahandisi ambao hawafanyi kazi na kukwamisha miradi ya maji nchini huku akisema utendaji kazi wa Ruwasa bado hauridhishi.
Awali, akisoma ripoti ya utekelezaji miradi wilayani Chamwino, Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini(Ruwasa) Chamwino, Christina Msengi amesema hadi Oktoba mwaka huu, watu 264,484 wanapata maji safi na salama sawa na asilimia 65 ya wakazi wote.
Amesema katika bajeti ya 2018/19, serikali ilitenga Sh.Milioni 350 kwa ajili ya kujichimba visima virefu katika vijijini 14 hadi sasa mkandarasi DDCA ameshalipwa malipo ya awali ya Sh.Milioni 175.1 na amechimba visima saba.
Ameeleza katika bajeti ya mwaka 2019/20, serikali kupitia Ruwasa Chamwino itaanza kukarabati miradi ya maji kupitia Mpango wa Malipo Kutokana na Matokeo (PbR) katika vijiji