Home Mchanganyiko Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa kwa kuwapeleka watoto wao  vyuoni.

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa kwa kuwapeleka watoto wao  vyuoni.

0

Baadhi ya wahitimu katika chuo Cha Veta Cha mafunzo ya hoteli na utalii kilichopo Njiro jijini Arusha  ambapo jumla ya wanafunzi 89 walihitimu kozi mbalimbali katika ngazi ya Cheti na diploma .
*************************************
Happy Lazaro,Arusha.
Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa kwa kuwapeleka watoto wao vyuoni   hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda ambapo kuna uhitaji mkubwa  wa  wasomi waliobobea viwandani.

Hayo yamesemwa Jana na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro wakati akizungumza katika mahafali ya Saba ya chuo Cha Veta Cha mafunzo ya hoteli na utalii ambapo jumla ya wanafunzi 89 walihitimu.
Muro amesema kuwa,katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima wazazi wachangamkie fursa ya kupeleka watoto wao vyuoni ambao watakuja kuziba nafasi mbalimbali za ajira katika mahoteli na hata viwandani.
“tatizo la watanzania wengi wakishaona viwanda na mahoteli yamejengwa kwa wingi ndo wataanza kupeleka watoto vyuoni ,na ndo maana nafasi nyingi za ajira kwenye viwanda na mahoteli zinachukuliwa na wenzetu kutoka nchi jirani kwani wao huwa wanajiandaa mapema na sio kusubiria waone  wapi pa kupata ajira.”amesema Muro.
Amesema kuwa,serikali ya awamu ya tano hivi Sasa haina mchezo ambapo nguvu kubwa inawekezwa katika uchumi wa viwanda na uwepo wake utasaidia sana idadi kubwa ya Vijana kupata ajira kwa haraka ,hivyo ni fursa kwetu kuchangamkia .
Mkuu wa chuo hicho ,Christopher Ayo amesema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikizalisha idadi kubwa ya wanafunzi kila mwaka ambao wamefanikiwa kupata ajira katika maeneo mbalimbali ,ambapo kimefanikiwa pia kuanzisha ushirikiano na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo chuo Cha utalii Kenya,na Nova Scotia Community College Cha Canada .
Ayo amesema kuwa,kupitia ushirikiano huo kimeweza kujenga uwezo mkubwa kwa Wafanyabiashara wake hususani wakufunzi na utawala ambapo kupitia ushirikiano wao na Nova Scotia wameweza kuandaa mitaala ya mafunzo ya uongozaji wa watalii na yale ya uendeshaji na utoaji huduma za kitalii na usafiri.
Ameongeza kuwa,chuo kupitia mradi wa ISTEP uliofadhiliwa na Canada wameweza kununua vifaa vya utalii Kama vile mahema,viwanda,vifaa vya Electronic na computer 20,ambapo vifaa vyote kwa ujumla vina thamani ya shs 63 milioni.
Ayo ametaja changamoto inayowakabili kuwa ni upungufu wa kumbi za mihadhara na madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi wengi, pamoja na kiwango kidogo cha majisafi na salama kinachopatikana,makazi ya watumishi na hivyo kukatisha masomo miongoni mwa wanachuo kutokana na matatizo ya kifamilia.
“kwa kweli.chuo chetu tumejipanga pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali pia, tuna mpango wa kuongeza udahili wa wanachuo Mia tano kwa mwaka kwa kozi zote,na pia tuna matarajio ya kuanzisha masomo kwa njia ya mtandao ili waliopo mbali na chuo waweze kujiendeleza .”amesema Ayo.
Kwa upande wake Mhitimu Madawa Pius   aliomba serikali kuongeza wakufunzi kulingana na uwezo wa chuo hicho,huku akiwataka wahitimu hao kukitangaza vyema chuo hicho popote watakapokuwa ikiwa ni pamoja na kutanguliza uzalendo mbele.