Home Mchanganyiko WENYEVITI WA MITAA WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI

WENYEVITI WA MITAA WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI

0

Viongozi walioteuliwa wakila kiapo mbele ya hakimu Elizabeth Justine (hayupo pichani) ili waanze majukumu yao.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa akiongea na viongozi wa serikali za mitaa walioteuliwa Halmashauri ya Mji Kondoa wakati wa zoezi la kuwaapisha.( Hawapo pichani)

Watendaji wa Mitaa waliohudhuria zoezi la kuwaapisha viongozi wateule wa serikali za mitaa

Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kondoa Michael Sanga akiongea na viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa hivi karibuni.

***********************************

Viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kutambua kuwa wameteuliwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si wananchi kuwatumikia wao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa wakati wa zoezi la kuwaapisha viongozi hao lililofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Nawapongeza kwa kuteuliwa kwenu ila nawashauri msiende kuwa miungu watu na wakali kwa wananchi pia mkaonyeshe ushirikiano kwa watendaji na wataalam katika maeneo yenu ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa wananchi,”alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha zliongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kwenda kuhakikisha kuwa wanakusanya mapato kwa kushirikiana na viongozi wengine kwani kwa jinsi watakavyokusanya fedha nyingi ndivyo watakavyopata asilimia 20 kubwa zaidi na kuwaletea maendeleo wananchi.

“Mkafanye kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili kuepuka kuingilia majukumu ya wengine na kurahisisha utendaji kazi na kubwa kwenu¬† ni kutatua migogoro ya wananchi na wajumbe mkawashauri vizuri wenyeviti wenu,”alisisitiza Mkurugenzi Dakawa.

Hata hivyo aliwataka Watendaji wa Mitaa kushirikiana na wenyeviti wao na wajumbe walioteuliwa kuhakikisha hadi kufikia mwezi Machi 2020 wawe wameandaa mpango wa ujenzi wa ofisi zao za mitaa.

Naye Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kondoa Michael Sanga aliwasihi viongozi hao kupeleka kwa Watendaji wa Kata au Mitaa makosa ya jinai ili wayashughulikie kisheria na kuepuka kukaa na fedha walizokusanya katika nyumba zao.

Awali akitoa taarifa ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kondoa Msimamizi wa uchaguzi Mwalimu Hassan Mtamba alisema kuwa jumla ya Wenyeviti 36, Wajumbe mchanganyiko 108, na Wajumbe Viti maalum 71 waliteuliwa baada ya kupita bila kupingwa na wote wametokana na Chama Cha Mapinduzi.

Zoezi la uapishaji viongozi hao limefanyika pamoja na utoaji semina elekezi kwa viongozi hao kutoka kwa wakuu wa Idara na ilihudhuriwa pia na watendaji wa Mitaa na waliapishwa na Hakimu Elizabeth Justine kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kondoa.