Profesa Kennedy Mwambeta Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Bonanza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa bonanza la kuhamasisha wana taaluma kufanya mazoezi wakati wote pamoja na upimaji wa afya kwa watu mbalimbali lililofanyika chuoni hapo leo.
Mkurugenzi wa mfunzo endelevu na Weledi MUHAS Dkt Doreen Mloka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mazoezi na namna ya kupata stamina ili kuendelea kufanya mazoezi kila siku.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wafanyakazi wa MUHAS wakiendelea na mazoezi katika uwanja wa chuo hicho leo jijini Dar es salaam
…………………………………………….
Pamoja na faida zinazotajwa ndani yaa mwili matumizi ya Pombe yamekuwa yanachangia ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutokana na wingi wa matumizi hayo na kupelelekea kupata shinikizo la damu, kiria tumbo, kisukari na mengineyo.
Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) Prof Andreas Barnabas Pembe wakati wa bonanza la kuhamasisha wana taaluma kufanya mazoezi wakati wote pamoja na upimaji wa afya kwa watu mbalimbali.
“Matumizi ya pombe si salama kwa afya ya mtumiaji kwani mtu akiwa anafanya mazoezi huweka mwili wake vizuri, ukingalia mtu anayekunywa bia moja au glass ya wine ni sawa na kula mkate kipande kimoja na hivyo kupelekea kuleta kiriba tumbio kwa mtumiaji.”
“tunaposema kiriba tumbo ni yale mafuta yaliyorundikana ndani ya mwili ambayo hayawezi kuchimwa kutokana na kazi zetu za kila siku, kwenye miaka ya 70 wanaume walionekana wengi wana kiriba tumbo ila kwa miaka ya karibuni wanawake wamekuwa wengi sana,”
Prof Pembe amesema, kama MUHAS kimewataka wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuondokana na maradhi yasiyo yakuambukiza pamoja na kiriba tumbo.
Amesema kuwa mazoezi ni kitu muhimu sana kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wananachi wenye magonjwa yasiyoambukiza ambayo sio mazuri kwa afya na wingi wa matumizi ya vyakula ambayo havina faids ndani ya mwili.
Mbali na kufanya mazoezi, kupima presha pia wameweza kutia ushauri elekezi kwa kufanya mazoezi ili kuyaepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza pia kutoa ushauri kwa wananchi kula chakula kulingana na kazi anayifanya mtu,”amesema
“Mtu anayefanya kazi ya kubeba mizigo mizito ni tofauti na yule anayekaa ofisini wanatakiwa na matumizi tofauti ya chakula kulingana na aina ya kazi anayofanya mhusika, na mara nyingi mtu anayetumia muda mwingi kukaa basi anatakiwa ale chakula kidogo,amesema Prof”
Mkurugenzi wa mfunzo endelevu na Weledi MUHAS Dkt Doreen Mloka amesema amefurahi sana kuwa moja ya washiriki wa mazoezi hayo ambapo amekiomba chuo hicho kuendelea kuandaa mabonanza kama haya mara kwa mara ili wajumuike pamoja kufanya mazoezi.
Amesema, hataishia hapa ataendelea kufanya mazoezi na kupungza kiribatumbo ambapo wameweza kupata elimu kuwa mazoezi ni afya na kwakua wanaanza mazoezi taratibu hadi pale watakapopata stamina.
Mwenyekiti kamati ya maandalizi wa bonanza hilo, Prof Kennedy Mwambeta amesema toka mwaka 2013 hakujawai kuwa na bonanza kama hilo na miaka yote wamekuwa wanaanza yale yanayowahusisha wanafunzi hususani pindi chuo kinapofunguliwa na kufungwa, ila kwa sasa wamejifunza kuwa jambo hili ni muhimu na litakuwa ni endelevu.
Bonanza hilo walilolipa jina la michezo kwa afya MUHAS limewahussisha wanataaluma wa chuo hicho na kufanya mazoezi ya aina mbalimbali na kupima afya zao. kisukari, shiniko la damu