Home Michezo MWAKINYO AMEMTANDIKA MFILIPINO KWA POINTI

MWAKINYO AMEMTANDIKA MFILIPINO KWA POINTI

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Mtanzania Hassan Mwakinyo ametumia vyema pambano lake la nyumbani baada ya kumgaragaza mpiganaji Arnel Tinampay kwa pointi baada ya kwenda raundi 10.

Mwakinyo alionekana kuzuia ngumi za mfilipino katika uso wake huku akitumia chansi kadhaa kuhakikisha anampiga sehemu ambazo zitampatia pointi na kuibuka mshindi katika pambano hilo ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa hamu na mashabiki kote ulimwenguni.

Kwenye utangazaji matokeo wa pambano hilo lilopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Jaji wa kwanza ametoa 97-93 , Jaji wa pili akatoa 98-92 na Jaji wa tatu akatoa 96-96.